• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Kikao kazi cha Wenyeviti wa Mitaa Manispaa ya Temeke

Posted on: December 23rd, 2019

WENYEVITI WAPYA MITAA 142 MANISPAA YA TEMEKE WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI, TARATIBU NA SHERIA ZA KAZI.

Hayo yamebainishwa leo katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Mitaa wapya wapatao 142 wa Manispaa ya Temeke, kikao ambacho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.

Kikao kazi hicho kilihudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwakilishi toka Takukuru, Mwezeshaji toka OR –TAMISEMI , Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Deogratius Lukomanya na Wenyeviti wa Mitaa yote inayounda Wilaya ya Temeke.

Akifungua kikao kazi hicho Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Felix Lyaniva amewataka wenyeviti wote walioaminiwa na wananchi wa Wilaya ya Temeke na kupewa ridhaa ya Kuongoza Mtaa wahakikishe wanatenda kazi kwa kuzingatia uwajibikaji, Uadilifu,Kuwa kiunganishi kwa wananchi, Utatuzi wa kero za Wananchi na kusimamia ipasavyo suala la Ulinzi na Usalama katika Mitaa yao.

“Akasisitiza kuwa Mwenyekiti wa Mtaa ndiye msemaji mkuu katika mtaa wake endapo majanga yoyote au maafa yametokea yeye ndiye mtoa taarifa hiyo natarajia kupata taarifa kutoka kwa Mwenyekiti hata nikipata taarifa hiyo toka kwa Mwananchi wa kawaida lazima nitampigia mwenyekiti wa Mtaa huo kupata uhakika wa jambo hilo” Alisema Mhe Lyaniva

Pia amewataka Wenyeviti katika mitaa yote kutokujihusiasha na mauziano ya viwanja au kitu kingine chochote kinacho fanana na hicho wafanye kazi za utawala na zile kazi za kiutendaji wawaachie watendaji wa Mitaa hii itasadia kupunguza migogoro isiyo ya lazima katika mitaa yetu.

Kwa upande wa TAKUKURU mwakilishi Bi Leticia amewaasa Wenyeviti hao kuzingatia takwa la kisheria linalohimiza utoaji taarifa za Rushwa TAKUKURU na kamwe wakiwa Wenyeviti wa Mitaa wasijihusishe katika kutenda Uovu wa aina yoyote, Uongozi wao usiwe sehemu ya kutoa au kupokea rushwa pia usiwe sehemu ya kujilimbikizia mali.

Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria kutoka OR-TAMISEMI Ndg Eustard A. Ngatale aktioa mafunzo kwa wenyeviti katika ukumbi wa mikutano Manispaa ya Temeke


Baada ya hapo mafunzo yalianza rasmi yakiendeshwa na Mwenzeshaji Ndg Eustard Athanace Ngatale Mkurugenzi msaidizi wa Sheria OR-TAMISEMI ambaye alianza kutoa semina ya mfumo wa uendeshaji wa Serikali za mitaa ambao umegawanyika katika makundi mawili kundi la watawala na watendaji hivyo kwa nafasi ya Mwenekiti yeye ni mtawala katika Mtaa wake.

Aidha aliwapa mafunzo ya  kanuni ,taratibu na Sheria za kazi katika Mitaa yao lakini pia mipaka ya nafasi zao kiutendaji na kubainisha majukumu yao katika kuwaletea Wananchi maendeleo katika ngazi za Mitaa.

Kwa ujumla Semina Kazi hiyo imeandaliwa na Manispaa ya Temeke Chini ya Uongozi wa Mkurugenzi Ndg Lusubilo Mwakabibi lengo hasa likiwa ni kuwapa uelewa wa majukumu yao ya kazi za kila siku Wenyeviti wa Mitaa ili waweze kuendana na kasi ya Mhe Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli ya Kuwaletea wananchi Maendeleo hasa Wananchi wa hali ya chini yaani wanyonge.


Baadhi ya Wenyeviti wa Mitaa wakifuatilia kwa makini wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke katika ukumbi wa Manispaa hiyo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke