• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Manispaa ya Temeke Kidigitali zaidi

Posted on: November 20th, 2019

TEMEKE KUTOKOMEZA UDUMAVU KWA WATOTO KIDIGITALI

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia idara ya afya jana imeandika historia kwa kuzindua program maalum ya kampeni ya kutokomeza udumavu kwa watoto ambayo mzazi au mlezi ataweza kupata maelekezo ya lishe bora na sahihi kwa mtoto kiganjani kwake  kupitia simu ya mkononi popote alipo.

Katika picha ni namna program ya Smart Growth Diary inavyoonekana ukifungua katika simu yako ya mkononi mara baada ya kupakua App yako.

Uzinduzi huo ulifanyika jana katika kituo cha afya Round table Kata Mbagala  Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wataalam wa afya wa kituo cha Round table,wanachi pamoja wadau wa mradi “Mentor” ambao ni TMDA ,TFNC,TAMISEMI na TdLab.

Baadhi ya kina mama wenye watoto wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa afya wakiongozwa na mgeni rasmi Bi Dorcas Mvinanka mwenye nguo ya kijani aliye mbeba mtoto wakati wa Uzinduzi.

Akizindua mfumo huo ujulikanao kwa jina la Smart Growth Diary “SGD” wenye kauli mbiu  Tokomeza udumavu Temeke kwa niaba ya Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke Ndg Dorcas Mvinanka ambaye pia ni katibu wa afya amesema kwa mujibu wa takwimu kila walipo watoto watatu mmoja anatatizo la udumavu nchini Tanzania.

Mgeni rasmi Bi Dorcas Mvnanka akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa program ya Smart Growth Diary katika hafla hiyo iliyofanyika kituo cha afya Round table Mbagala.

Kwa maana hiyo tatizo la udumavu nchini lipo na ndio maana Temeke leo tunazindua program hii ambayo itaenda kutokomeza tatizo hili kwa watoto wetu, na lazima tufahamu siku 1000 toka mtoto anapozaliwa ni muhimu kuzingatia lishe sahihi. Kupitia program hiyo mzazi au mlezi anachotakiwa kukifanya ni kuwa na simu ya mkononi smart phone atapakua App ya SGD akisha pakua App hiyo sasa atakuwa na uwezo wa kuuliza swali lolote juu ya lishe sahihi na atapatiwa majibu ndipo utaweza kujua ni chakula gani amuandalie mtoto wake kwa makuzi bora.

Katika kutumia program hiyo gharama kubwa ni bando tu na bahati nzuri wadau wetu wa Fabtech wameridhia kuendelea kuangalia changomoto za program na kuzitatua kwa kadri zitakavyojitokeza, na wamesema kwa siku za usoni wataangalia namna ya kuweza kutuma ujumbe ”SMS” ili hata wale wenye simu za kawaida waweze kupata huduma.

Kwa upande wa afiasa Lishe wa Manispaa ya Temeke Ndg Charles Malale amesema “tunapozungumzia udumavu kwa mtoto maana yake mtoto huyo amekosa mlo sahihi lazima tujue kutofautisha kati ya mlo kamili na mlo sahihi, tukisema mlo sahihi ni ule unaozingatia makuzi ya mtoto kimwili na kiakili katika malezi ya mtoto, tunashauriwa kuzingatia ushauri wa kitaalam zaidi. Rai yangu kwa wazazi wote wa Temeke tuitumie programa hiyo ili kutokomeza udumavu Temeke”.

Afisa lishe wa Manispaa ya Temeke Ndg Charles Malale akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa program ya Smart Growth Diary.

Aidha kwa upande wa mashuhuda wakazi wa Kata ya Mabagala ambao tayari wameshaitumia program hiyo ya Smart Growth Diary, wamesema ni nzuri na kwa kuwa waliweza kuitumia wakiuliza chakula gani cha kumpa mtoto kwa kuzingatia umri,uzito na urefu wake na kupata majibu kwa wakati. hivyo kwa wakazi wa Temeke ni fursa ya kipekee kwa wazazi/walezi wote kuitumia ili kutokomeza Udumavu.

#Tokomeza udumavu Temeke na Smart Growth Diary “SGD” kiganjani kwako…..

Temeke bila watoto wenye udumvu inawezekana

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke