• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Manispaa yaTemeke yajizatiti kuboresha miundombinu ya Elimu

Posted on: March 6th, 2019

Sekta ya elimu ni moja kati ya sekta muhimu sana katika kulisukuma gurudumu la maendeleo mbele. Afisa Elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa ngazi ya Sekondari BibiNeema Maghembeanabainisha hayo katika ufafanuzi alioutoa mapema leo.

“Kwa mwaka huu wa fedha wa 2018/2019, Idara ya Elimu Sekondari imefanikiwa kufanya mambo yafuatayo. Awali, kufanya ukarabati mkubwa wa miundombinu kwa shule za msingi ambapo tumekuwa na mpango mkakati na bahati nzuri tumekwisha kuanza kuomba vibali kwaKamishna wa Elimu TAMISEMI ili shule hizi ziweze kubadilishwa na kuwa za Sekondari, hii ni kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofaulu kila mwaka kutoka katika shule za msingi na kujiunga na sekondari.

Hivyo tumeanza ukarabati katika shule za msingi za Serengeti naMuungano ambapo tunatarajia kuziunganisha kuwa shule moja ya Sekondari. Ndani ya shule hizo tumefanikiwa kukarabati maabara tatu, chumba cha maktaba, matundu 23 ya vyoo (yanayohusisha wanafunzi, walimu, na wanafunzi wenye mahitaji maalumu) sambamba na ukarabati wa madarasa yasiyopungua 20.

Mpango huu unahusisha shule nyingine kama vile Shule ya Msingi Kibasila. Kwa shule hii itaendelea kubaki kama ilivyo yaani “Shule ya Msingi Kibasila” lakini shule hiyo imekuwa na zaidi ya madarasa takriban 33 ambapo madarasa 23 hayakuwa yanatumika. Madarasa hayo 23 yote yamekarabatiwa pamoja na miundombinu. Shule hii ya Msingi Kibasila pia, tumeiombea kibali kupandishwa hadhi kutoka shule ya msingi kwenda sekondari. Hivyo, ieleweke kuwa kilichofanyika ni kuchukua baadhi ya madarasa ya Shule ya Msingi Kibasila ambayo hayakuwa yakitumika na kuyakarabati tayari kutumika kama Shule ya Sekondari lakini Shule ya Msingi Kibasilia itabakia kuwa kama ilivyo,” anaeleza Afisa Elimu.

Anaendelea, “Ipo pia Shule ya Msingi Kilakala, ambapo kumefanyika ukarabati wa vyumba vya madarasa vipatavyo 12 pamoja na matundu 20 ya vyoo.

Halikadhalika ukarabati huu umefanyika kwa Shule ya Sekondari Charambe. Tumeweza kupata msaada wa kujengewa vyumba vya madarasa kutoka kwa wenzetu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) yapo madarasa matatu yanajengwa pale.

Halmashauri pia imeweza kulipa stahiki za walimu ikiwemo stahiki za fedha zao za likizo hivyo haya ni baadhi ya mambo ambayo kama Idara ya Elimu-Sekondari tumeweza kufanikisha.”

Shule za Sekondari za Kidato cha Tano na Sita

Afisa Elimu anasema kuwa, “Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina shule za sekondari za kidato cha tano na sita za Serikali zipatazo tatu. Shule hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Temeke, Shule ya Sekondari Kibasila na Shule ya Sekondari Chang’ombe. Shule hizi hazitoshelezi bado tunahitaji kuwa na shule za sekondari za kidato cha tano na sita za Serikalini ikiwezekana kila kata tuwe na shule za namna hii dhumuni likiwa ni kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaokwenda moja kwa moja katika elimu ya kidato cha tano na sita kupitia shule hizo zilizo ndani ya Halmashauri yetu.

Kwa sasa Halmashauri ina mpango mkakati wa kujenga shule za kidato cha tano na sita. Kwa mfano Shule ya Msingi Mbagala tunatarajia kuwa na kidato cha tano na sita pale lakini pia uboreshaji wa vyumba vya madarasa, miundombinu yote muhimu kwa ajili ya uanzishwaji wa shule ya kidato cha tano na sita.”

Changamoto

Moja ya changamoto inayoikabili Manispaa ya Temeke ni upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati. Kilio hiki ni cha taifa kwa ujumla. Kwa upande wa Idara ya Elimu Sekondari kwa Manispaa ya Temeke tuna uhitaji wa walimu wa somo la fikizia wapatao 115, na tulio nao ni 49 tu. Somo la Kemia tuna uhitaji wa walimu 119, tunao 65 tu. Somo la Baiolojia, tuna uhitaji wa walimu 150 walimu tulio nao 83. Na kwa upande wa walimu wa somo la Hisabati tuna uhitaji wa walimu 249 na tuna walimu 82. Kwa ujumla tuna uhitaji wa walimu 633 na walimu tulio nao 279, na kwa takwimu hizo maana yake tuna jumla ya upungufu wa walimu 354 katika masomo hayo yote.

Changamoto hii tunazitatua kwa kushirikiana na baadhi taasisi za elimu ya juu zilizopo ndani ya Manispaa ya Temeke mfano; Chuo cha DUCE kinafundisha walimu wa sayansi. Hivyo walimu wanaochukua masomo ya Sayansi kutoka DUCE tunawakaribisha katika shule zetu na kufanya masomo kwa vitendo (field teaching practices) na hivyo wanapokuwa katika kipindi hicho huwa tunawasambaza katika shule zetu zote na kwa kweli uwepo wao umekuwa ukisaidia kuziba mianya iliyokuwepo. Tumekuwa tukihakikisha kuwa kwa muda ambao tunakuwa nao hapa shuleni wanamaliza mada muhimu kwa kuangalia Mtaala (Syllabus).

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke