• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MKUU WA MKOA WA DSM ATAKA UFANISI ZOEZI LA USAJILI WA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

Posted on: November 28th, 2023

Na: Joanita Joseph - TMC Habari


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Albert Chalamila amewataka viongozi ngazi ya mkoa na wilaya zote jijini humu kusimamia na kuratibu kikamilifu utekelezaji wa mpango wa usajili na utoaji vyeti kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano katika mkoa wa Dar es salaam unaosimamiwa na Wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (RITA).


Ameyasema hayo leo Novemba 28, 2023 wakati akifungua mafunzo kwa viongozi wa mkoa na wilaya yanayolenga kutoa elimu na uelewa wa kina kuhusiana na mpango huo ili waweze kuratibu kwa ufanisi pindi utakapoanza kutekelezwa kwenye maeneo yao.


Mhe. Chalamila amebainisha kuwa takwimu zinaonyesha zaidi wa watoto Milioni 8.8 sawa na 60.8% jijini Dar es salaam wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa hiyo ni alama kuwa wakazi wa jiji hili wana uelewa juu ya umuhimu wa cheti cha kuzaliwa hivyo ni muhimu waendelee kuhamasishwa kutumia fursa hii kupata nyaraka hiyo muhimu.


"Cheti cha kuzaliwa kinasaidia sana kupata huduma za elimu, afya, ajira, mikopo na kupata nyaraka nyingine za utambulisho kama vile vitambulisho vya taifa pasi ya kusafiria na nyaraka nyingine.

"Aidha usajili wa vizazi unawezesha serikali kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga maendeleo na huduma za jamii." alisema Mhe. Chalamila


Halikadhalika amewataka viongozi kushirikiana na viongozi wa dini kutoa elimu kwa wananchi juu ya uwepo na umuhimu wa zoezi hili sambamba na kusimamia vema huduma hii isigeuzwe kuwa mradi wa kujipatia mapato kwa watu wachache.


Aidha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wake Mhe. Samia Suluhu Hassan na wadau wa maendeleo ikiwemo serikali ya Canada, Shirika la umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) na Kampuni ya mtandao wa simu Tigo kwa kuwezesha utekelezaji wa mpango huo.


Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Idd Nyundo Manispaa ya Temeke na kuhudhuriwa pia na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Uhamiaji, NIDA na UNICEF.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke