• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

NAIBU WAZIRI WS KAZI AWAJIA JUU WAWEKEZAJI WASIOFUATA SHERIA

Posted on: November 24th, 2022

Na:Shalua Mpanda

TMC Habari.


Wito umetolewa kwa wawekezaji Nchini kufuata sheria za kazi na katiba ya Nchi kwa Watumishi na kuacha kuwanyanyasa Watumishi hao kwa kuwa nia ya Serikali ni kuona Watanzania wananufaika na uwekezaji huo.


Hayo yameelezwa leo Novemba 24,2022 na naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kazi,ajira na vijana Mhe.Patrobas Katambi wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira ya kazi katika viwanda wilayani Temeke.


Naibu Waziri huyo amesema amechoshwa na malalamiko juu ya manyanyaso,ukatili na mazingira yasiyo rafiki kwa wafanyakazi na hasa katika viwanda vinavyomilikiwa na baadhi ya wawekezaji hapa Nchini.


"Hatuwezi kuzunguka kila kiwanda Nchi Nzima kuzungumzia suala moja kila siku,nawaagiza wawekezaji wote kufuata sheria za kazi na ile sheria kuu ambayo ni Katiba".Alisema Mhe.Katambi.


Mmoja wa wafanyakazi katika kiwanda cha kutengeneza mabegi cha Matrix International (T) Ltd kilichopo kata ya Keko amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa amefanya kazi zaidi ya miaka 10 katika kiwanda hicho bila ya kuwa na mkataba huku wengine wakilamika kuachishwa kazi bila kufuata utaratibu na kunyimwa stahiki zao.


"Yaani hapa unaingia asubuhi unafanya kazi mpaka saa 3 usiku au saa 4 na ikitokea siku umechelewa kufika asubuhi hata dakika 1 tu unakatwa elfu 1 na ukichelewa kufika kwenye kikao unakatwa elfu 5....ikitokea bahati mbaya umekanyaga "material"unakatwa elfu 50".Aliongeza mmoja wa wafanyakazi kiwandani hapo.


Pamoja na mambo mengine Mhe.Katambi ametoa muda wa siku 14 kwa wamiliki wa Kiwanda hicho kuhakikisha wanarekebisha changamoto zote zilizoelezwa na Wafanyakazi hao huku akiahidi kufuatilia maagizo hayo, mojawapo likiwa kuwapatia mikataba ya ajira Wafanyakazi hao wapatao 400.


Katika ziara hiyo ambayo naibu waziri Katambi aliambatana na katibu tawala wa wilaya ya Temeke Bi.Bupe Mwakibete ambaye alimuwakilisha Mkuu wa wilaya,pamoja na watendaji wengine kutoka NSSF,Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF),Wakala wa Afya na Usalama mahali pa Kazi(OSHA) walitembelea pia kiwanda cha Herocean Industries (T) Ltd.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke