• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Serikali Kumaliza Tatizo la Mafuriko Dar es Salaam.

Posted on: December 2nd, 2019


Waziri wa TAMSEMI  Mhe. Selemani Jaffo ameeleza mipango inayotekelezwa na inayokusudiwa kutekelezwa na serikali katika siku za usoni kwa ajili ya  kumaliza tatizo la mafuriko ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika jiji la Dar es Salaam.


Mhe. Jaffo ameeleza mipango hiyo mwishoni mwa wiki baada ya kukagua ujenzi wa mfereji katika mtaa wa Kijichi wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na serikali katika manispaa ya Temeke  kupitia Mradi wa Uboreshaji Miundombinu Jiji la Dar es Salaam (DMDP).


Akitoa ufafanuzi wakati wa mahojiano na waandishi wa habari  Mhe. Jaffo amesema kwamba kupitia DMDP takribani Kilometa 40 za mifereji mikubwa na kilomita 30 za mifereji midogo imeshajengwa, na kwamba kwa kiwango kikubwa mradi huo utaweza kuondoa changamoto ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.


''Kupitia mradi wa DMDP tumeamua kuboresha baadhi ya mito; mto Sinza,mto Cha'gombe ,hali kadhalika na mifereji,kwa mfano mfereji huu wa Kijichi, Lengo letu kubwa ni kuwa maji yote ya mvua ambayo huwa yanatapakaa  mitaani yaweze kwenda katika chaneli husika na kuweza kufika katika ukanda wa bahari kwa ajili ya kwenda kuingia baharini.


Sasa hivi tunaendelea na juhudi katika eneo la bonde la msimbazi, kuhakikisha kwamba tunaliimarisha bonde la mto msimbazi,lengo kubwa ni kwamba hatutaki kuona maji yanatapakaa katika jiji la Dar es Salaam .Imani yangu ni kuwa kazi hii ya awamu ya kwanza ambayo ni ujenzi wa mifereji imekamilika,na inaendelea kukamilika, katika baadhi ya maeneo lakini tutakapokuja kuanza 'package' namba 2 ,ile ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha kwamba bonde la Msimbazi tunaliimarisha vizuri,naamini kwamba jiji la Dar es Salaam litakuwa ni jiji rafiki kuliko jiji lingine lolote hasa katika suala zima ya usambaaji wa maji kwenye mitaa''. Alisisitiza Mhe. Jaffo.


Katika hatua nyingine Mhe. Jaffo amezungumzia suala la maji taka ambapo amesema kwamba  mpango wao mkubwa kwa kushirikiana  na wizara ya maji kupitia DAWASCO kupitia ni kuhakikisha kwamba  maji taka yanasafirishwa katika utaratibu mzuri. Na kwamba Sasa hivi wako kwenye 30% ,lakini mipango yao ya baadae ni kufika 75%. Ambapo  kupitia mpango mkakati wao  muda mrefu wataakikisha kwamba jiji la  Dar es Salaam  linakuwa jiji rafiki kwa watu kuishi.


Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na changamoto ya mafuriko hususani wakati wa mvua nyingi. Hata hivyo serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na mafurikio hayo kwa kuendelea kujenga na kuboresha miundondombinu ya kupitisha maji .


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke