• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

SIMULIZI YA ZAWADI ANTHONY YA MRADI WA PPP.

Posted on: August 25th, 2020

Na Faith Daniel.

Zawadi Anthony atatimiza miaka 33 mwaka huu. Ni mama wa watoto wawili wa kike, Asha na Jamila. Watoto hawa wanahitaji chakula, wanahitaji mavazi, na wanahitaji ada za shule. Mahitaji yote haya humtegemea Zawadi. Mume wa Zawadi ameendelea kuonekana nyumbani kwa nadra sana.

Ni saa tatu na robo asubuhi katika soko la Temeke Stereo, katikati ya mchanganyiko wa kelele wa wafanyabiashara na honi za magari na bajaji za mizigo; Zawadi anasikika akimgombeza dereva wa lori la mizigo kwa takribani dakika 10 kabla ya mbeba mizigo aliyesimama juu ya lori hilo kumshushia mkungu mmoja wa ndizi. Kichwani akiwa amebeba takribani kilo 30 za mkungu huo, Zawadi anaelekea kwenye eneo lake la biashara akiwa anatokwa jasho jingi mithili ya bomba la maji. Anafahamu bayana ingekuwa kazi rahisi kama angeweza kumlipa shillingi 500 mmoja wa wabeba mizigo (pota) ili wambebee mzigo wake lakini ni kiasi hichohicho anatakiwa kulipa kama ushuru kwa siku ya leo. Anafika na kushusha mzigo wake, na kuanza kuuburuza mpaka kwenye kizimba kidogo anachokaa kila asubuhi. Wafanyabiashara wengine jirani na yeye wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Wao walifika hapo sokoni alfajiri, wakati yeye akiwa nyumbani akiwaandaa watoto wake ili waweze kwenda shuleni. Sehemu aliyokaa kwa ajili ya kuanza biashara yake ya kuuza ndizi ni karibu kabisa na mtaro wa majitaka yaliyotuama, Zawadi anatikisa kichwa anapoisikia harufu ya uozo wa mchanganyiko wa matunda na mbogamboga vilivyoharibika kwa muda mrefu.

Mida ya mchana, maafisa wa biashara wanatangaza kuwepo na mkutano wa wafanyabiashara wote wa hapo sokoni na kuhimiza kila mtu kushiriki. Mkutano huo utakuwa jioni. Hadi muda wa kikao, Zawadi amefanikiwa kuuza takribani kilo 5 tu za ndizi. Kimoyomoyo anajisemea biashara haikuwa nzuri sana leo. Kwa unyonge mkubwa anasogea kwenye eneo la kikao pamoja na wafanyabiashara wengine. Afisa Masoko anawatambulisha maafisa kutoka Ofisi ya Manispaa ya Temeke, ambao wanawajulisha wafanyabiashara kuhusu ujenzi wa soko jipya la kisasa kando ya soko la sasa. Wakataarifiwa ujenzi umelenga kuongeza na kuboresha maeneo ya kufanyika biashara ikiwa ni pamoja na marekebisho ya miundombinu mbalimbali katika soko zima. Taarifa hizi zinamfurahisha sana Zawadi na wafanyabiashara wenzake ambao wanauliza maswali mengi na kutoa mapendekezo mbalimbali ili yazingatiwe katika ujenzi wa soko jipya. Wafanyabiashara wanazungumzia umuhimu wa kuwa na maegesho ya kutosha kwa ajili ya kushushia mizigo na maegesho ya vyombo binafsi vya wateja. Lakini pia wanakumbushia umuhimu wa uhifadhi na udhibiti bora wa taka ngumu na majitaka.

Mkutano unajadili pia maeneo ya kufanyia biashara kwa muda wakati ujenzi wa soko jipya unaendelea. Kadri mkutano unavyoelekea kufikia hitimisho, mmoja wa maafisa anauliza kama kuna mfanyabiashara yeyote wa kike mwenye maswali au maoni. Baada ya kimya kifupi, Zawadi ananyoosha mkono taratibu. Afisa anampa nafasi ya kuzungumza. Taratibu anaeleza kuwa anatarajia kuona ,mradi wa Soko Jipya unatenga maeneo  mengi na makubwa zaidi kwa ajili ya wanawake pale sokoni. Anaongeza kuwa kizimba chake cha sasa ni kidogo na kiko jirani sana na mtaro wa majitaka. Anaelezea kwamba hali hii inawakabili wanawake wengi wenye mitaji mdogo hapo sokoni ambao pamoja na kulipia shilingi 500/= kila siku bado mazingira ya wao kufanya biashara si rafiki hasa kipindi cha jua kali na mvua nyingi, hali hii inapelekea wateja wao wengi kutokufika sokoni na kusababisha mdororo mkubwa wa kibiashara. Wafanyabiashara wote wake kwa waume wanampigia makofi mengi Zawadi. Minong’ono inasikika miongoni mwa wanawake wakisifu jitihada zinazofanywa na Timu ya Uratibu Mradi kuwapa kipaumbele wanawake katika kuchangia mawazo yao. Anatarajia baada ya matengenezo ya soko, watakuwa na maeneo yenye nafasi za kutosha kuhifadhi na kuuza bidhaa zao. Anafikiria haja ya kupanua biashara yake kwa kuongeza viazi na vitunguu. Baada ya Mkutano Bi Zawadi anaianza safari ya kuelekea nyumbani akiwa na tabasamu mwanana la tumaini jipya!

Moja ya malengo ya Dira ya 2025 ni kujenga uchumi imara unaoweza kukabiliana na ushindani kutoka nchi nyingine. Ubunifu na ufanisi ni sehemu kubwa ya miradi ya PPP, na hivyo kuweza kutumika kurekebisha na kupanua miundombinu ya masoko. Uboreshaji wa Soko la Temeke Stereo utapanua wigo wa biashara na kuongeza fursa nyingi kwa vijana na akina mama, hivyo kuwahakikishia kipato cha uhakika na tumaini ya maisha bora zaidi. Timu ya Mradi ya Manispaa ya Temeke imeshirikisha na inaendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Zawadi kwa kipindi cha miaka miwili sasa.  Ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara, wakazi wa maeneo hayo na serikali za mitaa na kata, Manispaa imefanya mikutano mbalimbali ilikupata mawazo na mapendekezo yao. Simulizi ya Zawadi ni kati ya simulizi chache za watu ambao maisha yao yatabadilishwa baada ya mradi huu kukamilika. Ushirikishwaji wa wadau utakuwa ni zoezi endelevu wakati wote wa matengenezo ya soko na wakati wa uendeshaji wa soko baada ya ujenzi kukamilika.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke