• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Tahadhari ya Homa ya Dengu yatolewa.

Posted on: April 15th, 2019

Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitwavyo Dengue vinavyosambazwa na mbu aina ya Aedes . Mbu huyu anayeambukiza homa ya dengue hupendelea kuishi karibu na makazi ya watu na huweza kuuma binadamu mchana na usiku. Ugonjwa huu huathiri sana nchi za tropiko kama Amerika ya kusini na Africa. Ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa, hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue.

Kutokana na uwepo wa viashiria vya ugonjwa wa homa ya dengue, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia Idara ya Afya imechukua tahadhari kwa wakazi wake kwa kutoa elimu juu ya homa ya hiyo hususani kipindi hiki cha mvua na kuwataka wakazi kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote yanayotolewa katika vyombo vya habari ili kupata uelewa zaidi.

Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr.Gwamaka Mwabulambo alisema watu wanatakiwa kuchukua tahadhari ya homa ya dengue, na kubainisha kuwa dalili zake ni za wazi hivyo kuwataka wananchi kujikinga ili wasipate vimelea hatari vya homa vya dengue.

“Ugonjwa wa dengue ni hatari lakini bado tunaweza kujikinga na madhara yatokanayo na kuumwa na mbu huyo, na hatua madhubuti ni kuhakikisha  mavazi yanayovaliwa yanafunika miguu na mikono hususani nyakati za jioni na kuhakikisha mazalia ya mbu yanateketezwa ili kuondoa uwezekano wa kuzaliana zaidi”.Alisema Dr Gwamaka.

Alibainisha zaidi kuwa dalili za awali za ugonjwa huo ni pamoja na Maumivu makali ya kichwa macho kuuma, maumivu ya viungo, Kichefuchefu, kutapika, vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza, kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi.

Nae Bibi Prisca Uswege mratibu ufatiliaji wa magonjwa wa Manispaa ya Temeke alibainisha kwamba elimu inatolewa katika kata zote ili kuhakikisha mazalia ya mbu yanaharibiwa na alibainisha zaidi kwamba zoezi hili litakuwa endelevu kwa Manispaa yetu.

“Tunaweza kupambana na mbu hawa wa magonjwa endapo tutaamua kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kwa kuondoa vichaka na kufukia madimbwi”, Alisema Bibi Prisca.

Sambamba na hilo kupitia kikao cha Mganga Mkuu wa Mkoa, kamati ya ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko ilikuja na maazimio yafuatayo, kwanza kwa kuongeza nguvu zaidi kuangamiza viluilui, kushauri taasisi na maeneo yenye mikusanyiko ya watu kupulizwa dawa kuua mbu hawa, kutoa taarifa kwa waganga wafawidhi wa vituo ili wajiandae kama itatokea kupokea mgonjwa wa aina hiyo pamoja na  kupitia taaarifa za kila wiki za mfumo wa taarifa (eIDSR reports) ili kubaini vituo vyenye ongezeko lisilokuwa la kawaida la wagonjwa waliopimwa malaria, lakini hawakuonekana na vimelea vya malaria.

Ikumbukwe kuwa mara nyingi dalili za ugonjwa huu huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi. Dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili, lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za dengue.hivyo basi ni vema kuwahi kituo cha afya kwaajili ya vipimo na kubaini tatizo husika.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke