• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

TEMEKE YAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Posted on: November 30th, 2023

Na: Joanita Joseph - TMC Habari


Kila ifikapo Desemba Mosi,Dunia huadhimisha siku ya UKIMWI, lengo likiwa ni kuikumbusha Jamii kuhusu ugonjwa huu, kutafakari hatua zilizopigwa katika kukabiliana nao, kukumbuka na kuenzi mamilioni ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huu, lakini pia kutoa elimu na kuweka mikakati ya pamoja katika kudhibiti na kutokomeza VVU/UKIMWI.


Kuelekea kilele cha maadhimisho hayo leo Novemba 30, 2023,Temeke imeadhimisha siku ya UKIMWI Kiwilaya yaliyofanyika katika viwanja vya Zakhiem - Mbagala na kuhudhuriwa na Viongozi, Taasisi pamoja na Asasi mbalimbali.


Akizungumza wakati wa hotuba yake, Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, ametoa wito kwa vikundi Elimisha Rika, kuendelea kuelimisha jamii hasa kundi la vijana, kwakuwa maambukizi yanazidi kuongeza kasi kwa kundi hilo.


DC Mapunda ameonesha kuchukizwa na shughuli za mtaani almaarufu kama 'vigodoro', sababu zimekuwa chanzo cha kuleta maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI,ambapo amewataka viongozi katika serikali za Mitaa kudhibiti shughuli hizo.


"Tunatambua uhuru wa watu kufurahi, lakini furaha za kutuangamiza hazitufai, popote wanapofanya haya mambo wachukuliwe hatua za kisheria" alisema Mhe. Mapunda


Halkadhalika amekemea unyanyapaa kwa waathirika wa virusi vya UKIMWI, badala yake jamii iendelee kuwapenda, kushirikiana nao, na kuwasaidia kwa kadri inavyowezekana.


Katika hatua nyingine, Mhe. Mapunda amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kuhakikisha afua zote za kupambana na virusi vya UKIMWI zinapewa kipaumbele, sambamba na kutoa utaratibu wa utoaji mikopo kwa makundi ya Vijana, Wanawake na watu wenye Ulemavu.


Mwisho amepongeza na kushukuru wadau wote walioshiriki kufanikisha maadhimisho ya siku hiyo muhimu,na kuwataka wana Temeke kujiwekea utaratibu wa kupima afya katika kutokomeza UKIMWI ili kuishi kwa furaha.


Maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu ya jamii iongoze kutokomeza UKIMWI, yamewezeshwa na FHI 360, UMATI, MDH, PASADA, Untold foundation, PACT, N.K, yanatarajiwa kuadhimishwa Kimkoa kesho Desemba Mosi, 2023, katika manispaa ya Ubungo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke