• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Temeke yaungana na wadau kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani.

Posted on: June 5th, 2018


Manispaa ya Temeke imeungana na Manispaaa nyingine za Jiji la Dar es salaam katika sherehe za maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani,ambapo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.

Akitoa salam na pongezi kwa wananchi, Mgeni rasmi Makamu wa Rais  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliwataka wadau wa mazingira kuibeba kauli mbiu ya maadhimisho isemayo  ''MKAA NI GHARAMA,TUMIA NISHATI MMBADALA.''  kwa kuhakikisha inaleta  matokeo chanya.

''ninawataka wadau wa mazingira na wananchi kwa ujumla kuhakikisha utunzwaji wa mazingira pamoja na utunzwaji  wa miti ya asili unazingatiwa''

Katika hotuba yake Mama Samia alibainisha athari ziletwazo na utunzwaji mmbaya wa mazingira kuwa ni pamoja na kuharibu misitu ambayo itatusaidia kupunguza joto pamoja na hewa ya ukaa pamoja na bahari kuingia katika makazi ya watu,kukimbiza wanyama na wadudu , kuyeyuka kwa theluji  katika baadhi ya vilele vya  milima na ongezeko kubwa la joto duniani.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mazingira, Mheshimiwa January Makamba alisema maadhisho haya hufanyika kila tarehe 05/06 kila mwaka, lengo kuu likiwa kuwakumbusha wananchi utunzwaji wa mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo na kuwataka wadau na wananchi kusimama katika nafasi zao.

Akiwashukuru wadau wa mazingira kwa juhudi zao za kuhakikisha mazingira yanatuzwa kwa hali zote,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewataka kuhakikisha kampeni hii ni endelevu  ili kuokoa vizazi vijavyo dhidi ya janga la uharibifu wa mazingira

Pia amewataka wananchi wotewa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanazingatia agizo la usafi wa mazingira kila jumamosi ya kwanza ya mwezi na kutangaza tarehe 01/07/2018 kuwa ni siku ya usafi kwa Mkoa wa Dar es salaam.

Maadhimisho haya yamehudhuriwa na wadau na viongozi mbalimbali toka Manispaa zote pamoja na viongozi wa vyama vya siasa,pamoja na hamasa mbalimbali toka kwa wanamuziki waliohamasisha kwa tungo mbali mbali zenye ujumbe wa mazingira.



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke