• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

"TUTAPAMBANA NA KIPINDUPINDU KWA USAFI" MHE. AMOS MAKALLA

Posted on: March 25th, 2023

Leo Machi 25, 2023 Mkuu wa wilaya ya Temeke,Viongozi wa Chama,Watumishi wa Manispaa pamoja na watumishi wa Taasisi mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Amos Makalla wamefanya usafi katika eneo la Quality center hadi Tazara.


Akizungumza mara baada ya zoezi hilo la usafi, Mhe. Makalla amewataka Wananchi kujenga tabia ya kuchukia uchafu kwa kutokutupa taka hovyo ili kujiepusha na magonjwa hususani katika kipindi hiki cha mvua.


"Tukishakua na tabia ya kutokutupa uchafu hovyo naamini kabisa muda wote jiji letu litakua safi ili kuvutia watalii, wawekezaji lakini kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Juzi Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu Mhe. Simbachawene alikua anatoa mkakati ya kupambana na kipindupindu kitaifa, sisi Dar es Salaam tutapambana na kipindupindu kwa kuweka jiji letu safi na inawezekana" Alisisitiza Mhe.Makalla.


Aidha Mhe. Makalla ameagiza maeneo yaliyokatazwa kufanyika biashara kuheshimiwa ili kuacha Jiji safi na kuhakikisha maeneo hayo yanapambwa kwa bustani na miti. Alisema


"Watendaji wa Kata na Mitaa muendelee kusimamia maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara na kwenye 'road reserve' kuwe safi muda wote ili watu wapite. Niwaombe wadau tutunze mazingira yetu, tunakuja na kitu kingine katika Safisha Pendezesha Dar es Salaam kuhakikisha tunakuwa na bustani nzuri, tutapanda miti rafiki, tuhakikishe barabara hii inakuwa kijani"


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Mwanahamisi Munkunda amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa kiongozi bora kwenye suala la usafi, na kuwa Wanatemeke wanafanya usafi kwa hiari.


"Usafi ni 'mentality', usafi ni 'leadership' sasa watu hawalazimishwi wanafanya wenyewe kwa hiari, mpango wetu ni kuwaunga mkono viongozi wote kuanzia ngazi ya mtaa wanaounga mkono falsafa yako ya kuhakikisha kwamba Dar es Salaam linakua jiji safi na la kuvutia. Temeke ni lango la Kusini,tutaifanya iwe 'hub' ya usafi.'


Manispaa ya Temeke kupitia Viongozi wake inatoa wito kwa Wananchi wake kuhakikisha mazingira yao yanakua safi wakati wote ili kuzuia magonjwa ya mlipuko.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke