• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

TUWE NA UTARATIBU WA KUPIMA AFYA-DIWANI YOMBO VITUKA

Posted on: December 12th, 2022

NA; Sweetbetter Njige

TMC Habari

Leo Novemba 12,2022 ikiwa ni siku ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza ,Manispaa ya Temeke kupitia  Idara ya Afya  imeendesha zoezi la utoaji elimu juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ushauri juu ya masuala mbalimbali ya afya na upimaji wa afya bure.Zoezi hilo limefanyika katika hospitali ya Yombo Vituka .

Akizungumza katika uzinduzi  wa utoaji huduma, mgeni rasmi ambaye pia ni diwani wa kata ya Yombo Vituka Mheshimiwa Fulgence Rwiza aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa jitihada zake za kuwajali Wananchi kwa kuboresha huduma za afya, alisema.

"Niipongeze Serikali yetu hususani Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwalipia Wananchi wa Yombo huduma hii, leo huduma inatolewa bila malipo lakini Serikali yetu imelipia huduma hii kwa ajili yenu, niwaombe Wananchi wenzangu tuwe na utaratibu wa kupima afya zetu sio lazima uumwe ndio ukapime Malaria. Natamani tuelewe magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndiyo yanayotumaliza zaidi,hizi presha, kisukari ni hatari sana, tutunze afya na tuzingatie elimu tutakayoipata hapa"

Kwa upande wake mganga mkuu wa manispaa ya Temeke Daktari Irene Haule aliwata Wananchi kuachana na mitindo mibaya ya maisha na kuzingatia lishe bora, mazoezi na upimaji wa afya mara kwa mara.

"Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameanza kupewa kipaumbele, tutambue magonjwa haya yamekua mzigo mkubwa kwa Serikali kwasababu matibabu yake ni ghali sana mfano Saratani, lakini tukizingatia ulaji wa lishe bora, upimaji wa afya mara kwa mara na mazoezi tutafanikiwa kupunguza magonjwa haya"

Kwa upande wao Wananchi waliojitokeza kupata huduma wameishukuru Serikali kwa kutoa huduma bure na kuwajali watu wa rika zote,aidha wamkuushukuru uongozi na watumishi wa kituo hicho cha afya kwa huduma nzuri.

Wiki ya magonjwa yasiyo ambukiza imeambatana na kauli mbiu "Boresha mtindo wa maisha, boresha afya" ambapo Wananchi waliofanikiwa kufika walipata elimu juu ya magonjwa kama saratani ya shingo ya kizazi, magonjwa ya macho, masuala ya lishe na afya ya akili.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke