• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Wadau wa Mazingira Temeke Wapewa Elimu ya Kudhibiti Taka.

Posted on: March 30th, 2021

Elimu hiyo imetolewa na Asasi isiyo ya kiserikali ya "Lawyers Enviroment Action Team" kupitia Kongamano la Wadau wa Mazingira,lililofanyika mwishoni mwa wiki,katika ukumbi wa Darlive uliopo eneo la  Zakhiem,kata ya Charambe,wilaya ya  Temeke.

Katika Kongamano hilo lililowashirikisha wadau wote muhimu wa mazingira ambao ni  Maafisa Mazingira,Maafisa Afya,Watendaji wa Kata,Watendaji wa Mitaa,Wenyeviti wa mitaa,mama Lishe na Wamachinga,Afisa wa LEAT wakili Baraka Thomas aliendesha mafunzo kuhusu maana ya taka,sheria mbalimbali zinazosimamia suala zima la utunzaji wa taka,aina za taka( hapa alielekeza kuhusu makundi ya taka),

Washiriki walielezwa juu ya madhara yanayoweza kutokea kutokana na kutodhibiti taka.Sambamba na hilo,muwezeshaji alielekeza kwamba udhibiti wa taka unaanzia katika hatua ya ukusanyaji wa taka,ambapo alisisitiza kwamba ili taka ziweze kudhibitiwa vizuri,ni lazima katika ukusanyaji,taka hizo zitenganishwe kulingana na makundi yake.

Aidha alisisitiza kwamba ni muhimu kwa wananchi kuwa na elimu ya udhibiti taka,kwani kumekuwepo na uchafuzi mkubwa wa mazingira,ambao mara nyingi unafanywa na wananchi kwa sababu tu, ya kutokuwa na ufahamu wa kwamba kila taka inapaswa kudhibitiwa ama kuteketezwa kwa usahihi kulingana na kundi lake.Hapa Wakili Thomas alitoa mfano wa taka za 'Plastic' ambapo alisema kwamba taka hizo hazitakiwi kuchomwa moto,wala kuzikwa,bali zinatakiwakufanyiwa urejereshaji ( recirclering) kwani zinapochomwa moto, moshi wake husababisha madhara ya kiafya kwa viumbe hai,na vilevile huwa haziishi zote,na zinapozikwa/ kufukiwa chini haziozi,badala yake,zinasabisha uharibifu kwenye ardhi.

Wakili Thomas alitoa angalizo kwa washiriki hao kuhusu madhara ya kutokutunza mazingira ,ambapo àlisema "elimu ya udhibiti wa taka ni muhimu sana katika kuwawezesha wananchi kuhifadhi mazingira ,kwa sababu tusipohifadhi mazingira ,kwa siku zijazo,kuna viumbe watapotea.Tunadhibiti taka kutunza uhai wetu sisi na wa watu wengine".

Katika hatua nyingine wakili Thomas  alianisha misingi/kanuni za kimazingira ambapo kanuni ya kwanza ni kuchukua tahadhari,kabla ya kuteketeza taka.Kanuni ya pili,anayechafua mazingira ni lazima alipe.Kanuni ya tatu,anazalisha taka anapewa jukumu kubwa kuhakikisha kwamba taka anazozalisha,ama kuingiza nchini bidhaa ambazo zitazalisha taka,apewe jukumu kubwa zaidi katika uhifadhi ama uteketezaji wa taka hizo.

LEAT kupitia mradi wake wa kulinda haki za kimazingira kwa wanawake,vijana, wasichana na jamii kwa ujumla kupitia kuwezesha jamii katika masuala ya kisheria jijini Dar es Salaam imekuwa ikitekeleza mradi huo kwa kufanya shughuli mbalimbali,miongoni mwa shughuli hizo,ni kuendesha mikutano ya wadau ya kila wilaya kujadili hali ya kimazingira kila baada ya miezi mitatu na kutoa mafunzo kwa wanajamii kuhusu mazingira.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke