• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Wajasiriamali Kivutio Nanenane Banda la Manispaa ya Temeke

Posted on: August 6th, 2019

Waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akikagua kiatu kilichotengenezwa na kikundi cha SIMONS wakati alipotembelea banda la manispaa ya Temeke mwishoni mwa wiki. 

Wajasiriamali wa kikundi cha SIMONS group kinachojishughulisha na  utengenezaji wa bidhaa za ngozi, wamekuwa kivutio kikuwa kwa watu wanaotembelea banda la manispaa ya Temeke.Mvuto huo umedhihirishwa hasa na waziri wa Mifugo na uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ambaye baada ya kuona ubora wa viatu vinavyotengenezwa na kikundi hicho, ameahidi kukipa  kazi ya kutengeneza viatu aina ya buti jozi 200.


Akizungumza mara baada ya kauli ya Mhe. Mpina ,fundi mkuu na mshauri wa kikundi hicho ndugu David Josia Magumba amesema tamko la Mhe. waziri limetutia moyo sana,  tunaamini kwamba oda hiyo itatuvusha pakubwa sana,nikizingatia kwamba bado tuna uhitaji mkubwa sana wa pesa ,pesa tunayoipata bado ni ndogo, kiwanda chetu kinahitaji maboresho makubwa .


Magumba amesema kwamba  mpaka sasa hawajawa na soko la kutosha la bidhaa zao ,hali ambayo inawasababisha kushindwa kuzalisha bidhaa zao kwa wingi. Amesema kwamba kwasasa soko  wanalolitegemea ni mteja mmoja mmoja,hali ya kuwa wanauwezo wakuzalisha  bidhaa kwa wingi.Magumba pia amesema kwamba jitihada zinafanyika kuzungumza na wafanyabiashara  wanaouza viatu kwa jumla na baadhi ya wamiliki wa shule ili waweze kupata soko la viatu kutoka kwao.Magumba amesema kwamba masoko wanayoyalenga  kwa sasa, ambako ndiko walikoelekeza nguvu ni wanafunzi,vyombo vya ulinzi na usalama, wauzaji wa jumla na viwanda.


Aidha Magumba ameishukuru Manispaa ya Temeke kwa kuwapa fursa ya kuwepo katika maonesho ya Nanenane kwa mara nyingine tena ambapo amesema kwamba uwepo wao kwenye maonesho hayo ni fursa nzuri kwao kujitangaza,kutanua wigo wao wa masoko,  unawawezesha  kuonesha uwezo walionao ,vilevile kuwahamsisha wengine kuwa na uthubutu wa kujiunga kwenye vikundi na  kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya viatu,tofauti na ilivyo sasa ambapo watu wengi wanafikiri kwamba ili kuanzisha kiwanda cha viatu wanahitaji kuwa na mtaji mkubwa sana. Sambamba na shukrani hizo ,Magumba amemuomba Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Temeke, ndugu Lusubilo Mwakabibi awasaidie kuwatafutia masoko  ya viatu kwenye viwanda ,  kwenye jeshi la akiba la wilaya ( Mgambo) pamoja na shule.Sambamba na ombi hilo pia ameomba  kikundi chao kiwe na uwakilishi kwenye baraza la biashara la wilaya, ili kupitia  baraza hilo waweze kupata fursa zaidi ya kujitangaza.


Naye katibu wa kikundi,  ndugu  Sospeter Makunja  ametoa maoni yake ambapo amesema kwamba kama angepata nafasi ya kuonana na Mhe. Rais angemuomba awahimize Watanzania kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.Amesema kwamba wakati umefika sasa kwa Watanzania kuondoa fikra kuwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini hazina ubora ,kwasababu  wapo Watanzania kama wao SIMONS, ambao wanauwezo wa kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu kabisa.


Makunja  ameongeza kwa kusema kuwa wao kama Kikundi cha SIMONS wanaamini  kwamba kazi zao ni bora sana kwani hata baada ya kupata kupata ujuzi,  walijifungia kwa muda wa mwaka na miezi minne wakiwa wanabuni na kutengeneza bidhaa zao kabla hawajatoka nje rasmi kuzitambulisha kazi zao na kuendelea na uzalishaji.Na wamekuwa wakishiriki mafunzo mara kwa mara ili kujiongezea maarifa na ujuzi. 


Kikundi cha SIMONS  kilianzishwa mwaka 2016 kikiwa na jumla ya wanakikundi  5 na mtaji wa shilingi  4,000,000 ambayo ilitokana na wanakikundi wenyewe kuchanga.Kilianza rasmi kuzalisha bidhaa na kuziuza mnamo mwaka 2017.Bidhaa zinazozalishwa na kikundi hicho ni viatu vya ngozi aina zote , mikanda,mikoba,mifuko ,waleti na bidhaa nyinginezo nyingi za ngozi.Mpaka kufikia mahali walipo wameweza kuleta wataalamu mbalimbali kwa ajili ya mafunzo, ambapo hadi sasa wameshapata mafunzo mara 5,na jumla ya fedha kiasi cha shilingi 7,000,000, zimetumika katika kugharamia mafunzo hayo.Kwa sasa mtaji wao umefikia  shilingi   23,000,000.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke