• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

WANAFUNZI TEMEKE WALIOSHINDA OLIMPIKI MAALAMU KWENDA UJERUMANI NA RWANDA.

Posted on: February 9th, 2022

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mheshimiwa Abdallah Mtinika akiambatana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Elihuruma Mabelya wameshiriki zoezi la utoaji zawadi na medali kwa wanafunzi 27 na walimu wao walioshiriki katika mashindano maalumu ya olimpiki yaliofanyika mkoani Mwanza Disemba 13 mpaka 17, 2021 ambapo Temeke ilitoa washindi watatu wataokwenda nchini Ujerumani na Rwanda Juni 2022.

Katika hafla hiyo Mhe. Mtinika amewapongeza washiriki na washidi kwa kuiwakilisha na kuitangaza Temeke na Tanzania katika ramani ya dunia huku akiwapa kongole walimu kwa kufanya kazi kubwa na nzuri iliyoiletea Manispaa hiyo heshima.

"Halmashauri ya manispaa ya Temeke inafanya vizuri  Kila eneo hususan katika mapato, ujenzi wa madarasa, mazingira na michezo, hali ambayo inatokana na juhudi na ushirikiano mzuri baina yetu katika kuhakikisha manispaa hii inazidi kuendelea". Alisema Mhe. Mtinika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke  Elihuruma  amesema ni vyema kuandaa bajeti juu ya watoto hao ambayo itasaidia kuwawezesha na kuwatengeneza vijana hao ili waweze kushiriki michezo hiyo kwa ufanisi.

"Ninawaahidi Mstahiki Meya, Afisa elimu wilaya na Afisa elimu maalum tutafanya kila liwezekanalo katika bajeti zetu ili  kusaidia vijana hawa kwani kuna mahitaji mengi ya fedha ili kuwawezesha vijana hao". alisema Mkurugenzi Mabelya

Naye Afisa Elimu Maalumu Manispaa ya Temeke Bi. Tatu Salum amesema anashukuru  kwa michango ya wadau kufanikisha vijana  hao kushinda mashindano hayo huku akisema kuwa maandalizi yanaenda vizuri kwa wanafunzi wataoenda Juni 2022 na wengine 2023 nchini Rwanda na Ujerumani.

Nao wanafunzi vinara wa mashindano hayo Subira Mwinyimkuu na Yusra wamesema wamefurahishwa na uongozi wa Manispaa kwa kuweza kuwathamini na kuwatia moyo kwa kuwapa zawadi na kuahidi kwamba wataenda kujiandaa vizuri ili kuiwakilisha vyema Temeke na Tanzania nje ya nchi.

Ikumbukwe mashindano hayo yalijumuisha michezo ya riadha, mpira wa miguu, mitupo pamoja na mpira wa nyavu ambapo Temeke ilitoa wachezaji hao kutoka shule za msingi na sekondari mbali mbali za kundi maalumu na kufanikisha ushindi huo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke