• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

WANATEMEKE TUUNGANE, TUFANIKISHE JAMBO LETU KWA KISHINDO.

Posted on: May 10th, 2022

Na Sweetbetter Njige-TMC

Mwenge wa Uhuru ni moja kati ya alama muhimu za taifa la Tanzania,ambapo kwa mara ya kwanza uliwashwa katika kilelele cha mlima Kilimanjaro usiku wa Disemba 09,1961 kuashiria NURU,TUMAINI,HESHIMA na AMANI.

Serikali ya Tanzania ilianzisha mbio za mwenge wa Uhuru kwaajili ya kukusanya watu pamoja kushiriki katika shughuli za kisiasa,kijamii na kiuchumi, ambapo Mwenge huhusisha ukaguzi, uwekaji jiwe la msingi na ufunguzi wa miradi, unabeba jumbe za elimu na uhamasishaji , usikilizaji wa maoni na ushauri wa Wananchi waliofika katika miradi husika kwa ajili ya kuboresha mambo mbalimbali,unatoa ufafanuzi wa gharama zilizotumika kutekeleza miradi hiyo kwa namna nyepesi na kuhakikisha miradi inatekelezwa ipasavyo.

Kwa mwaka huu 2022, mbio za mwenge wa Uhuru zimezinduliwa mkoani  Njombe na mgeni rasmi, Makamu wa rais wa serikali ya awamu ya sita ,mheshimiwa  daktari Philip Isdor Mpango  Aprili 2, 2022.

Mkoani  Dar es Salaam, mwenge wa Uhuru umepokelewa  Mei 10, 2022 na katibu tawala  Ndugu Hassan Rugwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa  Mhe. Amos Makalla ,katika viwanja vya shule ya msingi Bunju A, wilaya ya Kinondoni.

Temeke ikiongozwa na mkuu wa wilaya Mhe. Jokate Mwegelo itaupokea mwenge wa Uhuru siku ya Jumamosi  Mei 14, 2022 katika ofisi za TAZARA na kuanza kuumbiza  katika maeneo mbalimbali Wilayani hapa kwa ajili ya ukaguzi na ufunguzi wa miradi ikiwemo;

  • Ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa shule ya sekondari Karibuni.
  • Wakala wa uuzaji wa Pikipiki-Taifa Kwanza.
  • Ununuzi wa Greda la Manispaa.
  • Ujenzi wa jengo la kujifungulia na upasuaji kinamama Zahanati ya Kilakala.
  • Ujenzi wa vyumba 13 vya madarasa na matundu 16 ya vyoo shule ya Msingi Goroka A.

Miradi iliyogharimu jumla ya shilingi za Kitanzania 1,488,520,778.00 kati ya fedha hizo, serikali Kuu imechangia shilingi 398,700,000.00  halmashauri ya manispaa ya Temeke imechangia shilingi 1,084,851,078.00 na  Wananchi shilingi 4,969,700.00.

Kama ilivyo ada mchumia juani hulia kivulini, shughuli za kuzindua miradi, zitafuatiwa na  mkesha utakaopambwa na buruduani mbalimbali  katika viwanja vya Zakheim- Mbagala, ambapo Wananchi na Viongozi  wataungana kufurahia juhudi na matunda ya ushirikiano unaosababisha maendeleo endelevu  katika wilaya ya Temeke.

WanaTemeke  tuungane ,tufanikishe jambo letu kwa kishindo tukibeba  katika kumbukumbu zetu nia njema ya kuhesabiwa ifikapo  wakati wa sensa  ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti kama inavyojipambanua  katika kaulimbiu yake.

Ujumbe wa  mbio za mwenge wa Uhuru  2022;

“SENSA  NI  MSINGI   WA MIPANGO  YA MAENDELEO; SHIRIKI KUHESABIWA, TUYAFIKIE MALENGO YA TAIFA”. 

TEMEKE IMARA, KAZI IENDELEE.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke