• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Watumishi Maafisa toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waitembelea Manispaa ya Temeke.

Posted on: June 10th, 2019

Watumishi Maafisa toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waitembelea Manispaa ya Temeke na kujifunza mambo mbalimbali ya kiutendaji hususani ugatuaji wa madaraka,masuala ya Elimu sambamba na mbinu za ukusanyaji wa mapato unaofanywa na Manispaa ya Temeke.

Akipokea ugeni huo Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Felix Lyaniva alisema amefurahishwa kwa jinsi ambavyo wageni hao wameamua kutoka Unguja-Zanzibar na kuja Bara hususani katika Manispaa ya Temeke kujifunza namna ya uendeshaji wa Manispaa na mafanikio kwa ujumla.


“Nimefurahishwa sana na namna ambavyo mmetufikiria,sio rahisi kuacha Manispaa zote na kuja kwetu , hakika kuna kitu cha tofauti mmekiona na kuamua kuja kujifunza,tumefurahishwa sana na jambo hili”.Alisema Lyaniva.


Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke ndugu Mwakabibi, alisema ninafurahishwa kwa jinsi ambavyo wageni mbalimbali wanavyoithamini Manispaa yetu na kuja kujifunza,urafiki huu wa kikazi utasaidia kujifunza mambo mbalimbali toka pande zote mbili kwa kubadilishana uzoefu.

“Sasa Temeke inazidi kuwa ya mfano, tumejionea wageni wengi toka Halmashauri mbalimbali nchini wakija kujifunza kwetu, na sasa imefikia mahali mpaka wageni toka visiwani wamepata habari njema za Manispaa na kuamua kuja kujifunza, hakika jambo hili linatia moyo sana katika utendaji wa kazi”.Alisema Mwakabibi.

Sambamba na hilo wageni walipata wasaa wa kuelekezwa namna Halmashauri yetu inavyofanikiwa katika suala zima la ugatuaji wa madaraka na mbinu za  ukusanyaji wa mapato .

Akitoa semina ya namna ya ugatuaji wa madaraka Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala ndugu Mrisho Mlela alisema sera ya ugatuaji wa madaraka imesaidia kwa kiasi kikubwa kwani imeongeza uelewa  na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

“Ni kweli kabisa ugatuaji wa madaraka umerahisisha uelewa wa wananchi wengi, karibu asilimia 90 ya kata zinaandaa na kuwasilisha mipango kwa kutumia mfumo wa fursa, pamoja na hayo serikali ina shule za sekondari za kata zipatazo 3,516 ambazo kwa sehemu kubwa zimejengwa kwa nguvu za wananchi hii inatupa faraja sana”.Alisema Mlela

Nae Afisa Elimu Msingi Bibi Dafroza Ndalichako alisema ugatuaji wa Elimu ya msingi na badaae Elimu ya sekondari ulitoka na tamko la Rais la tarehe 12/02/2008 kuhusu kugatua usimamizi na uendeshaji wa shule za Msingi na Serikali kutoka ilivyokuwa Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi kwenda kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM),kiutawala na idadi ya wanafunzi wanaofaulu  imekuwa ikiongezeka.
           Pamoja na hayo mhasibu wa mapato Bwana Harry Mbanga aliwaeleza wageni hao kuwa Halmashauri imebuni vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vimeifanya Manispaa kuendelea kujisimamia yenyewe katika masuala mengi ya uendeshaji wa Halmashauri , pamoja na hayo alibainisha kuwa Serikali imeweza kuboresha huduma za afya  kwa mwaka 2007 ambapo idadi ya vituo  ilikuwa 308 na kata zilikuwa 2500 lakini 2018/19 idadi  ni 4,420 ambapo vituo vya afya vimeongezeka hadi kufikia 535, pia  imejikita katika ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya vituo vya afya nchini na kuajiri wataalam wa afya, uboreshaji wa takwimu kwa kutumia mfumo kieletroniki (GOTHOMIS) pamoja kudhibiti makusanyo ya mapato katika vituo vya huduma pamoja na kuhimiza malipo ya kadi.


Nae Mkurugenzi wa Idara ya  Elimu ya Maandalizi na Msingi Zanzibar Bibi Safia A. Rijaal alimshukuru Mkurugenzi na watendaji kwa ujumla kwa  namna walivyopokelewa na masomo waliyoyapata yatakuwa chachu ya mabadiliko katika kuhakikisha wanasonga mbele.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke