• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA MRADI WA BRT-2 TEMEKE

Posted on: August 13th, 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Agosti 13, 2025 amefanya ziara ya kukagua Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Awamu ya pili (BRT -2) na Miundombinu yake katika Vituo Vikuu vya Mabasi hayo ikiwemo Kituo cha Mbagala Rangi tatu.


Waziri Majaliwa ametembelea Ujenzi wa Kituo maalum cha kujazia gesi kwa ajili ya Mabasi hayo kinachojengwa katika Kituo cha Mbagala Rangitatu ambapo Nishati hiyo ya gesi itatumika katika uendeshaji wa mabasi hayo takribani 257.


Awali ya Ziara hiyo ilianzia katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo Waziri Majaliwa ameona Shehena ya kwanza ya Mabasi 99 yaliyokwisha ingia Nchini.


Waziri Majaliwa akiwa Mbagala amesisitiza Mawasiliano ya karibu kati ya DART, Waendeshaji wa Mradi huo, OR-TAMISEMI pamoja  na Watoa huduma za kifedha upitia Kadi za Kielektroniki kufanya kazi usiku na mchana ili tu mara baada ya mabasi yote 257 kuwasili ndani ya mwezi huu Mradi uanze kutoa huduma iliyo ya kisasa, salama na haraka kwa Wananchi.


Halkadhalika Waziri Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) kuandaa Mchakato madhubuti utakaowezesha Madereva kuyaendesha Mabasi hayo kiufasaha kwa usalama wa Abiria na Chombo chenyewe.


Ziara hiyo imehudhuriwa na Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Zainab Katimba, Naibu Waziri OR-TAMISEMI, Katibu Mkuu kutoka OWM (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonaz, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda ambaye pia amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na Watendaji kutoka LATRA, NIT,  na DART.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • NINA IMANI KUBWA SANA JUU YENU- MD SATURA AWAFUNGUKIA WANAMICHEZO TEMEKE

    August 23, 2025
  • MICHEZO IKATUMIKE KUHAMASISHA UCHAGUZI MKUU 2025-MHE KATIMBA

    August 23, 2025
  • DKT. MACHELA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA KATA YA AZIMIO

    August 23, 2025
  • ACP MCHOME AONGOZA KIKAO CHA MTAKUWWA

    August 22, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke