• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Waziri Mpina Kushughulikia Bei ya Ngozi

Posted on: August 3rd, 2019

Waziri wa Mifugo na uvuvi Mhe. Luhaga  Mpina ameahidi kushughulikia bei ya ngozi ili iweze kuwanufaisha wafugaji  pamoja na na wazalishaji wa bidhaa za ngozi.Mhe. Mpina ameyasema hayo leo alipotembelea banda la halmashauri  ya Manispaa ya  Temeke katika viwanja vya maonyesho ya Nanenane  Morogoro. 

Akizungumza wakati akiangalia viatu vinavyotengenezwa  na wajasiriamali kutoka katika kiwanda kidogo kijulikanacho kwa jina la SIMONS kilichopo Kata ya Toangoma,Manispaa ya Temeke, Mh.  Mpina amesema''Msindikaji ananunua ngozi kwa mfugaji kwa sh. 1000  mpaka 3000,ngozi hiyo hiyo ikishasindikwa  inauzwa kati ya sh.   36,975 hadi sh.  127,500. Lazima tulishughulikie, kwa sababu kwa hali ilivyo sasa wazalishaji wa bidhaa za ngozi wananunua ngozi kwa wasindikaji kwa bei kubwa sana kitu kinachosababisha bidhaa za ngozi zinzozalishwa kwa kutumia ngozi ya hapa nchini kushindwa kushindana na bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ambazo bei zake zinakuwa chini kutokana na gharama zake za uzalishaji kuwa ndogo ". 

Mhe.Mpina amesema kwamba nilazima ifike mahali ngozi inayozalishwa hapa nchini iwanufaishe wadai wote wa ngozi kwani kwa jinsi ilivyo sasa ngozi haimnufaishi mfugaji kabisa. 

Akiwa katika banda la manispaa ya Temeke  Mhe.  Mpina ametembelea eneo la mifugo ambapo amejionea mifugo kama ng'ombe, kuku, bata, sungura, kuku na mbwa inayofungwa kwa kufuata kanuni za ufugaji bora. Vilevile ametembelea bwawa la samaki na bwawa la kuoteshea majani ya mifugo (Azolla) 

Kadhalika Mhe. Mpina ametembelea wajasiliamali wa Temeke  ambapo amejionea bidhaa za aina mbalimbali kama bidhaa  zitokanazo na mazao ya kilimo kama matunda yaliyosindikwa, mboga za majani zilizokaushwa, viungo vya chakula,uyoga,maharage,mchele,karanga na mafuta ya alizeti.  Bidhaa zitokanazo na kazi za mikono kama mikoba na waleti za kina mama, vikapu, hereni, bangili, mikufu, shanga na nguo. 

Aidha Mhe. Mpina ametoa pongezi nyingi kwa watu wote waliohusika kuandaa maonyesho ya Nanenane kanda ya Mashariki ambapo amesema kwamba kila mwaka kuna kuwa na mabadiliko, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa kuna kazi kubwa inafanyika kuyafanya maonyesho yawe bora zaidi. Mhe. Mpina pia amezipongeza halmashauri ambapo amesema kwamba halmashauri zote alizotembelea ziko vizuri sana, mabanda yamepambwa vizuri, yamependeza ,mifugo na mazao yako vizuri sana,  bidhaa zinazoonyesha pia ziko vizuri.

Mhe. Mpina amefanya ziara katika maonyesho  ya Nanenane kanda ya mashariki ambayo yanafanyika ndani ya manispaa ya Morogoro. Katika ziara hiyo Mhe. Mpina ametembelea mabanda mbalimbali likiwemo banda la halmashauri ya manispaa ya Temeke. 


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke