• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Ijue TARURA jinsi inavyofanya kazi katika Manispaa ya Temeke

Posted on: March 3rd, 2019


“Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) umeanzishwa chini ya Sheria ya Wakala wa Uanzishwaji wa Wakala za Serikali, Cap.125 na ulizinduliwa rasmi mwezi Julai, mwaka 2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Moja ya jukumu la Wakala huu ni kusimamia miundombinu ya barabara, jukumu ambalo mwanzoni lilikuwa likisimamiwa na Halmashauri zetu au Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hivyo jukumu hilo limetolewa rasmi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kukabidhiwa rasmi kwa TARURA. Majukumu ya kimsingi ni pamoja na matengenezo na ujenzi wa barabara mpya pale zinapohitajika.

Majukumu mengine ya TARURA ni kukusanya mapato yatokanayo na matumizi ya hifadhi za barabara katika barabara zetu zilizokuwa chini ya Serikali za Mitaa na jukumu hilo hufanyika katika kila ngazi ya wilaya,” Mhandisi Nicholaus anaeleza.

Miradi ya Barabara

Mhandisi anafafanua, “Tangu kuanzishwa kwa Wakala huu umefanikisha kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara:-

Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 tulitekeleza miradi ya barabara iliyokuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 8.8 za Kitanzania ambapo ulihusisha matengenezo ya aina mbalimbali (periodic maintenance), matengenezo ya mara kwa mara (routine maintenance) na matengenezo ya maeneo korofi (spot improvement) sambamba na hilo TARURA imefanikiwa kutengeneza madaraja na makalavati makubwa.

Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 tumeendelea na metengenezo ya barabara. Tulikuwa na bajeti ya Shilingi Bilioni 3.49 za Kitanzania ambazo zimetumika katika matengenezo ya barabara na tumekadiria kutengeneza kwa mwaka huu wa fedha zaidi ya Kilomita 80.2 ambazo zinapatiwa matengenezo ya aina mbalimbali yaani barabara zitakazokuwa kwa kiwango cha lami mfano: barabara ya Mbozi, Chihota, Masaki-Toangoma.

Pia tumekabidhiwa jukumu lingine la kusimamia baadhi ya miradi inayofadhiliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Miradi hiyo ni pamoja na ya DMDP ambapo tumekabidhiwa utekelezaji wa miradi hiyo isiyopungua kilomita 96 ambazo zinatarajiwa kutengenezwa ndani ya kipindi hiki. Miradi hii imegawanywa katika awamu, kuna awamu ya kwanza ambayo inaishia mwaka 2020 ambapo kutakuwa na utengenezaji wa barabara za kilomita 96 za kiwango cha lami na mifereji yake zikitekelezwa ndani ya kata 6 zilizopo katika Manispaa ya Temeke.Mwajiri wa Miradi hiyo atabaki kuwa Mkurugenzi wa Manispaa na TARURA inaendelea kuwa msimamizi pekee, hivyo tutaendelea kutekeleza miradi mingine inayofadhiliwa na Mfuko wa Barabara.”

Mhandisi anaendelea, “Kimsingi TARURA tangu ilivyoanza mpaka leo ipo katika kipindi cha mpito kwa hivyo kuna miradi mingi ambayo tumekuwa tukiitekeleza kwa ushirikiano wa karibu na Manispaa husika. Kwa mfano; Manispaa ya Temeke imekuwa na miradi mingi ya barabara ambapo inahamisha fedha kutoka vyanzo vya ndani kwa barabara zao ambazo wanadhani zina uhitaji wa kuboreshwa na kuzihamishia katika Mfuko wa TARURA kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara waliyoipendekeza. Kwa sasa TARURA imekwishapokea takriban Shilingi Milioni 200 za Kitanzania ndani kwa bajeti ya mwaka huu kwa minajili ya utekelezaji wa barabara ya Mchumila itayotengenezwa kwa kiwango cha .Changarawe

Pia, Manispaa ya Temeke ina jukumu la kuchangia ujenzi wa barabara ya Mbozi na tuna matarajio ya kupokea takriban Shilingi Bilioni 1.3 za Kitanzania kukamilisha mradi huo. Sehemu ya mradi huo unapata fedha kutoka Mfuko wa Barabara na fedha zingine zinatoka kwenye vyanzo vya ndani vya Mkurugenzi. Miradi ya namna hii iko miwili, Mradi wa Mbozi na Kiburugwa. Kwa Mradi wa Kiburugwa wenyewe unagharimu Shilingi Bilioni 1.8 za Kitanzania zinazotakiwa kutoka kwenye Ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya kukamilisha mradi huo.

Kwa Manispaa ya Temeke, Mtandao wetu wa barabara una kilomita 575.75 na hizo ni zile zilizotambuliwa na Mfumo wa sijaelewa kama lipo sahihi na kwa sasa bado zipo zingine ambazo tunaendelea kuziboresha. Kati ya hizo kuna kilomita takriban 59 za lami na kilomita 139 za kiwango cha changarawe na kilomita 376 za udongo ambazo tunaziboresha kuzipeleka katika changarawe na zile zilizo katika changarawe tunazipeleka katika kiwango cha lami.”

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke