• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

"ELIMU YA UCHANGIAJI DAMU IWE AJENDA YA KILA SIKU." DC Gondwe.

Posted on: November 21st, 2020

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Godwin Gondwe amewaagiza watendaji wa serikali wilayani humo kuendelea kutoa elimu ya uchangiaji damu.

Mhe.Gondwe ametoa agizo hilo mapema leo wakati wa hotuba yake kwa wana jumuiya ya Kiislam ya Jamii Yatul  Akhlaaqul Islaam (J.A.I)  na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwa wingi mapema asubuhi katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa kuchangia damu Mhe Gondwe amesema" Damu haina mbadala,huwezi kusema kwamba kwa sababu damu haipo tutafute jambo lingine tuweze kumwekea binadamu.Damu anayowekewa binadamu,inatoka kwa binadamu"

Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Godwin Gondwe akitoa hotuba katika hospitali ya mbagala rangi tatu wakati wa zoezi la uchangiajia damu.


Mhe Gondwe amesema kwamba mwaka 2019 upungufu damu katika hospitali ya Mbagala rangi Tatu ulikuwa kwa 49% ,lakini kuanzia Januari 2020 hadi mwezi huu,upungufu ni 18%, hali inayoonyesha kwamba elimu ya uchangiaji damu imetolewa,na wananchi wameelewa.Hata hivyo Mhe.Gondwe amesisitiza kuendelea kutolewa kwa elimu hiyo ambapo amesema" Wakuu wa Idara,Maafisa Tarafa,Watendaji wote,tukitoka kwenda kwenye kazi zetu za kila siku,elimu ya uchangiaji damu iwe  ni moja ya ajenda endelevu kuanzia sasa ndani ya wilaya ya Temeke"

Aidha Mhe Gondwe amewashukuru wanajumuia ya J.A.I kwa kuuona uhitaji,na kuamua kuchangia damu,amesema  kwamba wamefanya kazi nzuri na ya kutukuka,na amezitaka jumuiya zote wilayani Temeke kuiga mfano kwa jumuiya hiyo ambayo imeonyesha kujali na kuthamini maisha ya watu. Katika hatua nyingine Mhe. Gondwe amewapongeza Wanatemeke kwa   kuelewa,na kuona umuhimu wa kuchangia damu,jambo ambalo limewezesha kupungua kwa changamoto ya upungufu wa kiasi cha damu kinachohitajika.

Taasisi ya J.A.I imeendesha zoezi la uchangiaji damu katika hospitali ya  Mbagala Rangi Tatu,hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kutekeleza zoezi hilo katika mkoa wa Dar es Salaam.Ambapo imeweka historia ya kipekee kwa kuanzia katika wilaya ya Temeke.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke