• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

IDARA YA MAENDELEO YA JAMII MANISPAA YA TEMEKE YAGUSWA KUSAIDIA WATOTO WENYE UHITAJI

Posted on: January 18th, 2024

Na: Joanita Joseph -TMC Habari


Watumishi kutoka Idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya manispaa ya Temeke katika kutekeleza majukumu yao leo Januari 18, 2024 wamefanya matendo ya huruma kwa jamii kwa kutembelea kituo cha watoto yatima wenye ulemavu kiitwacho Human Dreams Children's village kilichopo Mikwambe kata ya Tuangoma wilayani humu.


Watumishi hao kupitia idara hiyo wamekabidhi bima za afya 35 zenye thamani ya shilingi elfu arobaini kwa kila moja, unga wa lishe, siagi, maziwa pamoja na kiasi cha fedha kutoka katika sehemu ya mishahara yao ikiwa ni sehemu ya kuchangia mahitaji ya kila siku kwa watoto hao.


Akizungumza katika ziara hiyo Bi. Furaha Chiwile, Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Manispaa ya Temeke ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kusaidia watoto wenye uhitaji lakini pia kwa wazazi kutunza watoto kama hao endapo watapatikana kwenye familia yao.


"Jamii tunapopata changamoto ya watoto tusiwatupe, tuangalie namna gani ya kuwalea badala ya kuwatelekeza, tuzingatie maelekezo tunayopewa na wataalam wa afya katika kutunza ujauzito ili mtoto asipate matatizo pindi atakapozaliwa. Lakini pia nitoe wito kwa wadau kutembelea vituo vya watoto wenye mahitaji maalum kama hivi" Alisema Bi Furaha.


Nae Emmanuel Hillary, msimamizi wa kituo hicho ametoa shukrani kwa idara hiyo na halmashauri kwa ujumla kwa kuwawezesha msaada huo huku akiiomba Serikali kuendelea kusaidia vituo kama hivyo ukizingatia utunzaji wa watoto hao unahusisha gharama kubwa.


Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2015 na mama Nicole mtawa mwenye asili ya kijerumani mpaka sasa kinahudumia jumla ya watoto 48 ambapo 33 wanaishi na kutunzwa kituoni hapo na 15 wanakuja kwenye huduma ya mchana (day care).


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke