• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

LEAT KUTOA ELIMU YA MAZINGIRA KIBURUGWA

Posted on: August 13th, 2021

Kamati ya mazingira wilaya ya Temeke pamoja na Maafisa kutoka LEAT wakiwa katika ziara kutembelea maeneo yenye  changamoto za kimazingira.

Kamati ya mazingira wilaya ya Temeke pamoja na Maafisa kutoka LEAT wakiwa katika majumuisho,mara baada ya ziara.


Kamati ya mazingira wilaya ya Temeke kwa kushirkiana na Maafisa kutoka katika asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira ( LEAT), leo  Agost 13,2021 wamefanya ziara katika kata ya Kiburugwa iliyopo manispaa ya Temeke.


Lengo la ziara hiyo ni kuangalia changamoto mbalimbali za kimazingira zilizopo katika eneo hilo na kuzitafutia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo ambayo kamati hiyo chini ya ufadhili wa LEAT ukifanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kata hiyo,ambapo ilijionea changamoto zilizopo, ikiwemo kubomoka kwa nyumba za wakazi wa maeneo  hayo,hali ambayo husababishwa na mafuriko yanayotokea kila msimu wa mvua.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, diwani wa kata ya Kiburugwa Mheshimiwa Fatuma Shija ameishukuru LEAT pamoja na kamati hiyo kwa kufika katika Kata yake,na kwamba anaamini kuwa ujio huo utakuwa ni chachu ya utatuzi wa changamoto za kimazingira zilizopo katika eneo hilo,ambazo ni nyingi sana.

"Nashukuru mmefika katika kata yangu,kata ya Kiburugwa ina changamoto nyingi za kimazingira,ujio wenu ni faraja sana kwangu,na kwa Wananchi wa eneo hili,kwani naamini kwamba kwa kushirikiana, sisi,ninyi LEAT pamoja na wadau wengine, changamoto mlizozibaini zitapatiwa  ufumbuzi" Alisisitiza Mhe. Shija.

Naye Afisa wa LEAT ambaye pia  ni mratibu wa mradi,wakili Teresia Fabian ameeleza hatua watakazochukua baada ya changamoto walizoziona ili kutatua,ambapo amesema"Tumetembea ,tumeona,kama ambavyo  Mhe. Diwani amesema,changamoto ni kubwa,kuna suala la ujenzi holela wa makazi hapa,ambao kutokana na huo , hata ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji katika eneo hili ni mgumu, pili ardhi ya eneo hili ni changamoto kubwa kwani ni ya kichanga,ukichanganya na kutokuwepo kwa mifereji ,pamoja na sehemu ya eneo hili kuwa bonde,ambalo tumesikia hapa kwa wenyeji kwamba bonge hili limesababishwa na shughuli ya uchimbaji wa  mchanga ambayo ilikuwa ikifanyika miaka 30 iliyopita, imesababisha eneo hili kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara, ambayo yanasababisha nyumba kubomoka na uhalibifu wa mali nyinginezo za wakazi wa eneo hili,ikiwemo samani .

Vile vile imesababisha kuwepo kwa makorongo katika baadhi ya maeneo,ambapo ili kuziba makorongo hayo ,taka zimekuwa zikitumika.

Tutakachokifanya kwanza ni kutoa elimu kwa Wananchi wa eneo hili.Tutaangalia pia na msaada mwingine tutakaoweza kutoa.

Kuhusu takataka kutumika kufukia makorongo,wakili Fabian amesema kwamba  sheria za Mazingira haziruhusu kufanya hivyo,lakini wamekwisha shauriana na Mhe. Diwani pamoja na maafisa Mazingira wa Manispaa,kuhusu chakufanya katika eneo la Kwashego ambalo limegeuzwa eneo la kutupia taka(dampo),kwamba litafutwe greda, eneo Hilo lisawazishwe,kisha vimwagwe vifusi,visambazwe, lipandwe majani ( ukoka) na miti.Lakini pia ulinzi uimarishwe,ili watu wasiendelee kutupa taka.

Naye Afisa Mazingira wa manispaa ya Temeke bibi Fina Benard amesema kwamba wameona changamoto zilizopo katika eneo hilo,atafikisha taarifa kwenye ngazi husika,na kwamba anaamini suluhisho litapatikana.

Mkoa wa Dar es Salaam kama ilivyo kwa baadhi ya mikoa hapa Nchini, una changamoto  nyingi za kimazingira.LEAT kupitia mradi wake wa kuelimisha wanawake vijana na jamii kwa ujumla kuhusu haki ya kuishi katika mazingira safi na salama,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  wa Mazingira pamoja na Manispaa za Mkoa huo  imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali  kupunguza changamoto hizo.Miongoni mwa shughuli wanazozifanya ni kutembelea maeneo yenye changamoto ,kubainisha changamoto hizo na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • LIPA USHURU WA HUDUMA ZA HALMASHAURI June 21, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WATUMISHI WA VITUO VYA KUKUSANYAJI MAPATO WASHIRIKI HAFLA YA PAMOJA

    June 21, 2025
  • MANISPAA YA TEMEKE YAPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA NI MARAFIKI NA JIJI LA YONGKANG-CHINA

    June 20, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAACHA ALAMA,LAIDHINISHA MIRADI LUKUKI KUTEKELEZWA 2025/2026

    June 20, 2025
  • NAPA YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA UTEKELEZAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

    June 20, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke