• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MAMIA YA MAMA NA BABA LISHE TEMEKE WAKABIDHIWA MAJIKO NA MITUNGI YA GESI

Posted on: March 7th, 2024

Na: Joanita Joseph -TMC Habari


Katika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi na bora ya kupikia Nchini.


Leo Machi 7, 2024 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Nchini Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Biteko amekabidhi mitungi ya gesi aina ya 'ORYX' na majiko kwa mama na baba lishe takribani 100 wilayani Temeke ikiwa ni katika utekelezaji wa mpango wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wa nishati safi ya kupikia Afrika aliouzindua katika mkutano wa dunia mnamo mwaka jana 2023.


Dkt. Biteko amesema kuwa ni muhimu kuweka mkakati maalum wa kutumia nishati safi ya kupikia ili kuepuka madhara ya kiafya kutokana na matumizi ya nishati isiyo safi.


"Safari ya nishati safi ya kupikia imeanza rasmi hapa nchini, tunataka tuwaone akina mama wa kitanzania wanahama kwenye matumizi ya nishati isiyokuwa safi, na nishati safi ili uweze kuifikia ni lazima serikali ifanye uwekezaji na uwekezaji umeanza. "Alisema Dkt. Biteko.


Vilevile Dkt. Biteko ametoa rai kwa viongozi wa serikali pamoja na taasisi kuipa uzito agenda ya nishati safi ili kuboresha maisha ya Mtanzania na maendeleo hapa Nchini.


"Niendelee kuziomba kampuni nyingine zinazozalisha mitungi ya gesi ama nishati nyingine zisibaki nyuma, wafanye kila wanaloweza kuhakikisha watanzania wanapata nishati safi na wanapata maendeleo". Alisema Dkt. Biteko


Aidha Dkt. Biteko ametoa ahadi juu ya umalizaji wa tatizo la upungufu wa umeme kwa wakazi wa mbagala.


"Ninyi wenyewe mmekuwa mashahidi kwa miezi hii miwili hatujafanya mgao wa umeme, hivyo niwaahidi suala hili linakwenda kwisha hivi punde kwakuwa uboreshaji tayari umeshaanza na muda si mrefu unakwenda kukamilika." Alisema Dkt. Biteko


Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam Mhe. Albert Chalamila amemshukuru Mhe. Naibu Waziri hususani katika utatuzi wa changamoto za Nishati hapa Nchini.


"Naibu waziri Mkuu wewe umesimama imara sana katika kuhakikisha sekta unayoisimamia haya malalamiko yote yanakwisha au yanapungua kwa asilimia kubwa sana ". Alisema Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam.


Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya zakhiem, Mbagala wilayani Temeke.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke