• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Manispaa ya Temeke ilipotoka, ilipo katika ukombozi wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu

Posted on: January 7th, 2020

Katika kuhakikisha maisha ya wananchi wa Temeke yanaboreshwa na kwa kuzingatia agizo la Serikali linatekelezwa kutokana na  azimio lililotolewa na kikao cha  Bunge  cha mwezi Agosti 1993 kuwa, Halmashauri zote nchini zitenge na kupeleka asilimia kumi (10%) ya mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani kwenye mfuko wa kuendeleza Wanawake na Vijana.

Manispaa ya Temeke ilipoanzishwa mwaka 2000 iliendelea na utoaji wa mikopo kwa wanawake na vijana kupitia Kamati ndogo za mikopo zilizoundwa katika ngazi ya Kata na kuratibiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii Kata na kupitishwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).Katika kipindi hiki Halmashauri ilipata hasara kubwa kwani wakopaji wengi hawakurejesha kama ilivyokusudiwa ingawa jitihada kubwa ilifanyika ikiwemo kuajiri wakala (TAPSE) ili kudai madeni hayo.

Kufuatia hali hiyo Halmashauri iliamua kufuta madeni hayo.Mnamo mwaka 2015 Idara ilitoa mapendekezo ya uratibu wa mikopo kupitia benki ya DCB na baada ya kupitishwa na Kamati ya Fedha na Uongozi, Benki hiyo ilianza kutoa mikopo hiyo kwa niaba ya Halmashauri kuanzia Septemba 2016 hadi Juni 2018.

Kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 Halmashauri ilitenga jumla ya shilingi milioni mia nane sabini na sita laki tatu na elfu tatu mia tisa ishirini na moja na senti tisini ( 876,303,921.90) ambazo zilipelekwa  Benki ya Wananchi wa Dar es Salaam (DCB) ili benki ikopeshe kwa niaba ya Halmashauri. Fedha zote zilikopeshwa kwa jumla ya vikundi 387 ambapo vikundi  203 ni vya Wanawake na 184 vya Vijana. Fedha hizi  ambazo ni za mzunguko(revolving fund) ziliendelea  kukopeshwa hadi mwaka uliofuata.

Mwaka 2017/2018 Halmashauri ilipeleka kiasi cha shilingi milioni mia tatu (300,000,000/=) benki ya DCB na kufanya jumla ya fedha zote za kukopesha jumla ya vikundi 357 ambapo vikundi 189 ni vya Wanawake na 168 vya Vijana kufikia kiasi cha shilingi 1,176,303,921.90.

Kutokana na utaratibu wa utoaji mikopo kuanzia 2016/2017 na 2017/2018 fedha ya mkopo ilikuwa katika mzunguko (revolving) na kuweza  kukopesha jumla ya kiasi cha shilingi bilioni moja,milioni mia nane themanini na nne na laki nne( 1,884,400,000).


Mwaka 2018 Halmashauri ililazimika  kutekeleza agizo la waraka wa TAMISEMI unaozitaka Halmashaurin zote nchini kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu bila riba.Agizo hilo  lilitokana na AMMENDMENT OF THE LOCAL GOVERNMENT FINANCES ACT (Cap 290)  sheria ya Fedha  namba 4 ya  mwaka 2018  kutenga asilimia 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kukopesha  makundi hayo.

  •  

Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana iliwasilisha mapendekezo ya namna ya kutoa mikopo katika kikao cha Menejimenti cha tarehe 6.11.2018. Baada ya majadiliano ya kina kati ya kwenye menejimenti ilipendekezwa kwamba mikopo hii itolewe kwa vikundi ambavyo vina miradi inayofanana ambavyo vitaunganishwa ili kutengeneza kundi kubwa litakalowezeshwa kwa kupatiwa vifaa kulingana na aina ya shughuli wanazofanya.

Idara na Menejimenti (CMT) zilipendekeza kuwa mikopo hii iratibiwe katika ngazi ya Halmashauri kwa kuwapatia wanavikundi vitendea kazi ili kupata tija zaidi kuliko fedha taslim

Miradi iliyopendekezwa kulingana na mazingira ya Temeke ni pamoja na:

  • Ufyatuaji wa matofali
  • Mradi wa kutengeneza madaftari
  • Mradi wa ushonaji nguo
  • Miradi ya kutengeneza viatu
  • Usindikaji wa matunda ya msimu
  • Miradi ya Usafi(uzoaji taka/Fumigation)
  • Miradi ya utengenezaji wa samani
  • Miradi ya bustani
  • Miradi ya ufugaji wa Samaki
  • Miradi ya kutengeneza sabuni za usafi

 

Halmashauri hadi kufikia  Juni 2019, kiasi cha  Tshs 24,867,353,293 kiliweza kukusanywa ikiwa ni mapato bila vyanzo lindwa.

 Kulingana na mapato hayo   kiasi cha Tshs. 2,486,735,329 kilitolewa   kwa ajili ya mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambayo ni asilimia kumi (10) ya mapato ya ndani.  Asilimia 4 ya wanawake ni Tshs. 994,694,131.6          asilimia 4 ya vijana ni Tshs. 994,694,131.6 na asilimia 2 ya watu wenye  ulemavu ni  Tshs.  497,347,065.8


Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwa mwaka 2018/2019 imeweza kutoa mikopo kwa njia ya vifaa badala ya fedha taslim. Mikopo ya vifaa iliyotolewa kwa vikundi 16 vya wanawake ,vikundi 10 vya vijana na vikundi 18 vya watu wenye ulemavu wenye  ni Fedha hizi  za manunuzi ya vifaa  zinafikia  jumla kiasi cha Tsh 2,001,976,723  kwa  44.


 

 Aidha, Katika kipindi cha Oktoba – Disemba 2019 kumekuwa na ongezeko kubwa la vikundi vinavyoomba mikopo ya fedha taslim, hasa kwa wafanyabiashara ndogondogo (mama lishe).

Kamati ya Fedha na Uongozi ilipitisha utoaji wa mikopo ya fedha taslim kuanzia Tshs 100,000- 2,000,000 kwa kikundi. Mpaka sasa kiasi cha Tshs. 42,000,000 imeandaliwa kutolewa kwa ajili ya vikundi 38.

 

Kwamwaka 2019/2020 Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya kukopesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.Hadi kufikia Disemba 2019 kiasi cha Tshs 660,107,743 kimetumika  na kufikia  jumla ya  shilingi 2,662,084,466/= kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu tangu ilipoanza kutolewa mwaka 2018/2019.

.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke