• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Manispaa ya Temeke inavyotumia Kodi kuwa daraja la Maendeleo kwa wananchi

Posted on: March 5th, 2019


Manispaa ya Temeke ni moja ya Halmashauri tano zinazounda Jiji la Dar es salaam, Manispaa nyingine ni Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni .Manispaa ya Temeke ina eneo la kilometa za mraba 240 na ukanda wa pwani kwa kilometa 5.

Manispaa ya Temeke ipo upande wa kusini mwa Jiji la Dar es salaam ambapo kwa upande wa Mashariki inapakana na Manispaa ya Kigamboni pamoja na bahari ya Hindi, kusini inapakana na Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, na upande wa Kaskazini na Magharibi inapakana na Manispaa ya Ilala.Wilaya kongwe katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Kihistoria Temeke ndiyo Wilaya ya kwanza hapa Dar es Salaam na ni Manispaa ambayo ipo Kusini Magharibi mwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kulingana na sensa ya watu na makazi ya  mwaka 2012, Manispaa ya Temeke ilikuwa na jumla ya watu 1,205,949 na kaya 307,760. Kati yao wanaume walikuwa 587,857 na wanawake walikuwa 618,092. Mpaka mwaka huu 2019 Manispaa ya Temeke inakadiriwa kuwa na watu wapatao 1,579,498 na kaya 431,711. Kati yao wanaume ni 769,949 na wanawake 809,549.Mpaka sasa Manispaa ya Temeke ina idadi ya watu takriban Milioni 1.8 na tunakwenda kufikia Milioni 1.9.

Temeke inakaliwa na watu wa hali zote, kuanzia wale wenye kipato cha chini, wenye kipato cha kati na hata wenye kipato kikubwa, ndiyo maana huwa tunapenda kusema Temeke ni “Wilaya ya Wananchi.”

Kitu kizuri kuhusu Temeke ni kuwa ni moja ya Halmashauri ambayo imebeba takribani makabila yote ya hapa nchini. Watu wengi wanavutiwa kufanya makazi Temeke ndiyo maana idadi ya watu ni wengi ukilinganisha na Manispaa zingine.

Asilimia kubwa ya Watanzania ni watu wa mpira hivyo linapokuja suala la wapi unaweza kwenda kuburudika kwa aidha mechi za Simba na Yanga au Taifa Stars, basi huna budi kusogea pale Uwanja wa Taifa ambao upo pia ndani ya Manispaa ya Temeke.

Kama ambavyo Mamlaka na taasisi zingine zimekuwa zikijaribu kuonesha namna ambavyo zimekuwa zikiunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo, vivyo hivyo Manispaa ya Temeke nayo inatualika kufahamu shughuli za kimaendeleo zilizotekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa ndani ya mwaka wa fedha 2018/2019.

Shughuli hizo zimegawanywa kulingana na baadhi ya idara zilizopo ndani ya Manispaa hiyo ambazo ni Afya, Elimu, Fedha na Biashara na Ujenzi

Afya

Sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta muhimu sana hivyo kwa kutambua umuhimu huu, Manispaa ya Temeke imeendelea kusimama kidete kuhakikisha afya za wakazi wengi wa Manispaa hiyo zinaboreshwa.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Gwamaka Mwabulamboanaelezea jitihada hizo.

  • Ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya

“Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Idara ya afya ndani ya Manispaa ya Temeke imeendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi wa Chama tawala kwa kujenga zahanati kwa kila Kijiji na Vituo vya afya kwa kila kata ambapo kwa mwaka huu tayari tumeshajenga zahanati moja eneo la Kijichi, imekamilika na tumeshaifungua. Zahanati hii kwa baadaye itakapokuwa na idadi toshelezi ya wahudumu wa afya itafanya kazi kama Kituo cha Afya.

Pia, Idara imekuwa na majukumu mengine kama upanuzi wa vituo vya afya. Kuna ujenzi unaoendelea wa jengo la ghorofa tatu katika kituo cha afya cha Yombo Vituka, ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 60 na tunategemea mwaka huu utakamilika.

 Sambamba na hilo Yombo Vituka, tumepata fedha kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) fedha ambazo zimesaidia kujenga majengo matatu, jengo moja la utumishi, chumba cha kufanyia upasuaji (Operating theatre) na wodi ya akina mama na Watoto.

Mpaka sasa majengo yote matatu yamekamilika na nyumba ya MtumishiInatumika. Wodi ya akina mama na watoto imeanza kutoa huduma lakini kwa upande wa chumba cha kufanyia upasuaji tunatarajia kuanza kutoa huduma za upasuaji ndani ya mwezi huu wa februari baada ya kupata vifaa tiba kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD).”

Dkt. Mwabulambo anaendelea, “Tunayo Zahanati yetu ya Buza ambayo watu wamekuwa wakipatiwa  huduma lakini kuna ujenzi wa jengo la ghorofa tatu chini ya ufadhili wa fedha za DMDP ambapo linatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2019. Mara baada ya kukamilika kwa jengo hilo kutakuwa na huduma mbalimbali kama vile huduma za kulaza wagonjwa, huduma za upasuaji, huduma za Maabara na baada ya kukamilika kwa taratibu zote tutaibadilisha zahanati hiyo na kuwa Kituo cha Afya.

Idara imeendelea na uboreshaji wa Zahanati mfano; Zahanati ya Majimatitu kupitia fedha za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo tumefanikiwa kujenga majengo ya maabara, majengo ya upasuaji, na wodi ya akina mama na watoto, ujenzi ukiwa umekamilika kwa asilimia 100. Jengo la Maabara na wodi ya akina mama na watoto yameanza kutumika lakini chumba cha upasuaji kinasubiri vifaa ambapo inatarajiwa ndani ya mwezi huu wa februari vitakuwa vimefika. Upasuaji utakaofanyika ndani ya Zahanati hiyo ni upasuaji wa mama wajawazito na wagonjwa wengine lengo ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi (Mama wajawazito na watoto wachanga).

Pia, tunaratajia ndani ya mwaka huu kufungua maeneo ya kufanyia upasuaji manne ndani ya Manispaa ya Temeke. Kuna Kituo cha Afya cha Roundtable ambacho hakikuwa kikitoa huduma ya upasuaji kwa muda mrefu kutokana na ukweli kuwa chumba chake cha upasuaji (theatre) hakikuwa kimekidhi vigezo vinavyotakiwa, hivyo tumeshafanya ukarabati pamoja na kuwekea vifaa nayo tunatarajia ndani ya mwezi huu wa februari kuanza kufanya kazi. Kwa Bajeti hii hii inayoendelea, tumepanga kununua gari la kubebea wagonjwa (ambulance) moja, na tayari fedha zimeshalipwa. Tunamshukuru sana Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa amekuwa akilitilia uzito sana suala hili kiasi ambacho alipoingia tu ofisini kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kununua gari hilo na muda wowote gari hilo litawasili.”

  • Watumishi wa afya

Dkt. Mwabulambo anabainisha, “Kwa kweli si tu kwamba tuna upungufu wa wauguzi bali tuna upungufu wa watumishi wa kada mmbalimbali. Kwa sasa tuna watumishi 802 huku mahitaji yetu ni kuwa na watumishi 1,236 (upungufu wa watumishi wa asilimia 27). Mahitaji yataongezeka kwa kuwa tayari tuna ujenzi wa vituo vikubwa maeneo ya Buza na Majitatu hivyo hata mahitaji yao yataongezeka.

  • Huduma za afya kwa wazee

Hili ni jambo ambalo lipo katika mipango yetu na tayari tumeweza kuwatambua wazee 10,537 katika kata zote na wazee hao ambao tayari wamekwisha tambuliwa na Manispaa watapatiwa vitambulisho vya matibabu. Hivi vitambulisho vitakuwa vinawasaidia wanapokwenda katika vituo vyetu vya afya kuweza kutambulika na kutibiwa bure kama ambavyo Sera ya Wizara ya Afya inavyoelekeza kuwa, “Mzee yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 60 anatakiwa kutibiwa bure” hivyo tumeweza kulizingatia kwa namna hiyo.

Zoezi hili litakuwa endelevu ambapo kila mwaka tutakuwa tunawatambua wazee na kuwapatia vitambulisho vya matibabu. Ningependa kutoa rai kwa wazee wanaopatiwa vitambulisho hivyo kuwa makini navyo na kuvitunza kwa sababu tumeshawahi kuwa na kesi za wazee waliopoteza vitambulisho hivi. Hali hiyo imekuwa ikitupa ugumu sisi kuanza kudurufu upya vitambulisho vya wale waliopoteza.”

 

Ujumbe

“Naomba tuendelee kushirikiana hasa wananchi katika miradi yetu ya afya. Na tunawashukuru kwa kweli wananchi kwa kujitoa kwao, kuna kamati zimeundwa ambapo wananchi wamekuwa wakijitolea kusimamia ujenzi wa vituo vya afya kwa asilimia 100 bila ya malipo yoyote na bado tunawasihi waendelee kuchangia katika miradi mbalimbali ili fedha zitokazo Serikalini ziweze kumalizia sehemu kubwa inayobakia,” Dkt. Mwabulambo anaweka nukta.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke