• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MASHINDANO SHIMISEMITA YAZINDULIWA RASMI

Posted on: October 24th, 2022

Nassoro Rashid

TMC Tv

Leo Oktoba 24, 2022 kaimu mkuu wa mkoa ambaye pia ni  mkuu wa wilaya ya Malinyi Mhe. Mathayo Masele amezindua rasmi mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa Tanzania(SHIMISEMITA) katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro na kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya, mwenyekiti SHIMISEMITA Taifa, TAMISEMI pamoja na washiriki mbalimbali.

Katika uzinduzi huo uliowashirikisha wachezaji kutoka  Halmashauri 44 za wilaya pamoja na manispaa nchini umeonesha hamasa kubwa kwa Viongozi, Watumishi pamoja na Wananchi waliohudhuria  kwa kuona jinsi gani michezo ni sehemu ya maisha ya kila siku.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa Mhe. Masele amesema wana furaha kubwa mashindano hayo kufanyika Morogoro, na ameahidi kutoa ushirikiano kwa  washiriki  mpaka watakapomaliza mashindano hayo, huku akiwashukuru waratibu wa mashindano hayo kwa kuiweka Nchi katika ramani ya michezo kwa Watumishi.

"Nimeambiwa mashindano haya ni ya 37 tangu kuanza kwake, niwaombe nyie mliofika muendelee, kwani michezo ni afya, urafiki na uchumi, tuendelee kumshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutujali wanamichezo lakini pia kuzijali afya za Watumishi". Alisema Mhe. Masele

Naye Mwenyekiti wa SHIMISEMITA Taifa  amesema walianza mashindayo hayo rasmi Oktoba 18, na wanatarajia kumaliza ifikapo Oktoba 31, 2022 huku akitoa rai kwa Viongozi wa Halmashauri kupanga bajeti mapema ili mashindano ya mwakani yawe katika hali nzuri zaidi.

"Bahati nzuri tunao viongozi wa TAMISEMI hapa ,tunawaomba katika bajeti mbali mbali zinazopelekwa na Halmashauri, kipengele cha kukipa uzito unaostahili kuona je watu hawa afya zao zinalindwa namna gani kwa kuweka bajeti katika kipengele cha SHIMISEMITA". Alisema Mwenyekiti

Mashindano haya yameibua hisia kubwa kwa Watumishi wa serikali za mitaa mara baada ya miaka 8 kupita huku yakionesha matumaini makubwa ya kuimarisha afya, uchumi na uhusiano kwa watumishi ikiwa yataendelea kupewa kipaumbele kila mwaka nchini.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke