• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

Milioni 189 kunufaisha wanawake Temeke.

Posted on: October 23rd, 2019


Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva amekabidhi gari pamoja na vifaa vya kuzolea taka,vyenye thamani ya shilingi 189,000,000 kwa  jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kata ya Miburani.

Tukio hilo la makabidhiano ambalo limekwenda sambamba na uzinduzi wa gari lililokabidhiwa limefanyika katika viwanja vya ofisi za manispaa ya Temeke.

Akizungumza kabla ya  kukabidhi gari pamoja na vifaa hivyo, Mhe. Lyaniva amewaasa wanajukwaa wa Miburani kuendelea kushirikiana katika kufanya kazi,kushirikiana kutunza gari pamoja na vifaa  na kuendelea  kuwaheshimu viongozi na wataalamu wa manispaa kwani wao ndio waliowawezesha kufika mahali walipofika.

'' Muwe kitu kimoja katika kufanya kazi,  mmepewa gari na vifaa hivyo, huo ni mkopo usio na riba, mmepewa miaka 3 ya kurudisha,mkishindwa kurudisha,maana yake ni kwamba mkopo huo unarudi, wanapewa watu wengine.

Mimi naomba mshikamane,muwe kitu kimoja, mmeshapata vifaa, mmeshapata gari, msije mkafika mahali mkawa hamsikilizani tena, mnawadharau wataalamu wa Manispaa ambao ndio wamewawezesha kupata mkopo huu.''

Akionyesha kufurahishwa na tukio hilo Mstahiki Meya wa manispaa ya Temeke Mhe. Abdallah Chaurembo  amesema kwamba mkopo waliopewa hauna riba, washirikiane kuhakikisha kwamba wanamaliza kulipa,ili gari hiyo iwe ya kwao, waendelee kuifanyia kazi iwasaidie kujikwamua kiuchumi.

Naye Mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ndugu Lusubilo Mwakabibi amesema kwamba yeye pamoja na wasaidizi wake watafuatilia utunzwaji wa gari hilo ili  liweze kufanya kazi iliyokusudiwa na kuwanufaisha wanawake hao kiuchumi.''Alisisitiza Mhe. Lyaniva.

Katika hatua nyingine diwani wa kata ya Miburani Mhe. Juma Mkenga ameshukuru kwa wanawake wa kata yake kupata mkopo huo, ambapo amesema kwamba upatikanaji wa vifaa vivyo utawezesha kazi ya uzoaji taka ngumu kufanyika kwa  wepesi na kwa ufanisi zaidi.Vile vile amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Temeke kwa kutoa wazo la kuanzisha ukopeshaji wa vifaa kwa vikundi vya ujasiliamali,kwani wazo hilo ndilo liliwezesha upatikanaji wa vifaa hivyo.

Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kata ya Miburani ni miongoni mwa majukwaaa yaliyoanzishwa na makamu wa Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan, Lengo la majukwaa hayo ni kuwaunganisha wanawake ili wawe na sauti moja yenye nguvu,ya kuwawezesha kutambua fursa mbalimbali za kiuchumi na kuwawezesha kutatua changamoto za kiuchumi zinazowakabili.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke