• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

MKUU WA IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA TEMEKE AHIMIZA UPANDAJI MITI.

Posted on: February 9th, 2022

Siku ya Januari 28,2022 Mkuu wa idara ya usafi na mazingira manispaa ya Temeke Bw.Ally Khatib kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Jokate Mwegelo ameendesha zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na Taasisi ya ‘Raleigh Tanzania Society’ katika shule ya  sekondari Dovya iliyopo kata ya Chamazi wilayani Temeke.

Katika zoezi hilo  Khatib alieleza umuhimu wa zoezi la upandaji miti katika shule na mazingira mengine kwa ujumla huku akifafanua sababu iliyofanya kupanda miti ya matunda.

“Tunaishukuru sanataasisi hii ya Raleigh kwa kushirikiana nasi katika zoezi hili la upandaji miti,mnafahamu hali ya mabadiliko ya tabia ya Nchi na namna yanavyoathiri mazingira yetu kwa kugundua hili tumekutana hapa na kupanda miti mbalimbali hasa ya matunda ambayo sio tu itatoa kivuli kwa watoto wetu wakiwa shule bali itatunza mazingira na kutoa matunda kwaajili ya afya”.Alibainisha Mkuu huyo wa Idara

Pia alitoa wito kwa wanafunzi hao kutunza  miti hiyo huku akisisitiza kuanzisha na kuendeleza desturi ya utunzaji mazingira hasa mashuleni.

“Katika mikakati ya utunzaji mazingira tumeanzia na shule kwasababu itakua desturi, hapa ni mahali ambapo vijana wetu wanapata elimu ya utunzaji mazingira na mazoezi ya kutunza miti waliyoipanda wenyewe na kuendeleza desturi kwa jamii. Natoa wito, hasa kwa wakazi wa Temeke tuhakikishe tunapanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira yetu ambayo kwa kiasi yameharibiwa na shuguli za watu za kila siku".Aliongeza Bw.Khatib

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Raleigh Bi. Karen Khan alifafanua nia ya upandaji miti katika shule na mazingira mengine tofauti.

“Kupitia kampeni ya mazingira inayoitwa “Kesho Tutachelewa” tunaendesha zoezi la kupanda miti ,tumejikita katika kuleta mabadiliko binafsi katika utunzaji mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Tunaamini mazingira bora yanahamasisha elimu bora,wanafunzi watapata chachu ya kutunza mazingira na kuwa na uelewa mzuri kwamba wanapaswa kutunza mazingira ili kukabiliana na changamoto za kimazingira”.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari Chamazi na mlezi wa ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari Dovya Mwalimu Emetrudius Chilewa alisema.

“Tunawashukuru sana Raleigh na viongozi wa wilaya ya Temeke kwa kutuletea miti na naahidi miti hii yote itatunzwa, wanafunzi hawa waliopanda hii miti wataitunza na watajivunia kwasababu kila mti hapa utaitwa jina la huyo mwanafunzi” alisema Mwl. Chilewa.

Nao wanafunzi wa shule hiyo kupitia mwakilishi wao Mohammed Alli mwanafunzi wa kidato cha kwanza alisema

“Asanteni kwa kutupandia miti na kutambua shule yetu haina miti,tunajarajia kupata kivuli,matunda na tunashukuru Mhe. Rais kwa kutujengea shule nzuri,tumeipenda na tunafurahi kusoma hapa bila kubanana”

Wilaya ya Temeke imekua mstari wa mbele katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa kusimamia usafi na upandaji miti ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke