• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA UEZEKAJI KWA DC TEMEKE.

Posted on: February 9th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo siku ya Februari 03, 2022 amekabidhiwa vifaa vya uezekaji na benki ya NMB vyenye thamani ya shilingi 13,000,000 katika hafla fupi iliyofanyika shule ya msingi Keko Magurumbasi yenye lengo la kuisaidia kuezeka baadhi ya madarasa ya shule hiyo na shule ya msingi Buza zilizopo wilayani Temeke.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Jokate amewashukuru sana wadau wa benki ya NMB kwa mchango huo na kujitoa kwao katika kuchangia maendeleo mbali mbali katika jamii na kuwa wadau wakubwa kwa kushirikiana na kumuunga Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.

Pia ameongezea kwa kuwaomba benki ya NMB kutokuishia hapa katika kujitolea na kuwataka waendelee kushirikiana katika kujenga jamii ziwe bora zaidi ili wao waendelee kutimiza malengo yao na serikali itimize malengo yake kwani wote wanajenga nyumba moja kwa ajili ya Tanzania.

Kwa namna nyingine Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Mhe. Rais amewekeza kiasi kikubwa katika kuboresha miundombinu itakayoendeleza sekta ya elimu kwa sababu inagusa maisha ya watoto na vijana.

"Kwa sababu ukishika elimu, ukiboresha elimu unawasaidia vijana kukua katika malezi bora lakini pia kuwasaidia kuwa na maono juu ya maisha yao, kwahiyo Mhe. Rais amewekeza moyo wake katika kiwanda ambacho kinazalisha watoto na vijana ambao Taifa linaenda kuwategemea" Alisema Mhe. Jokate.

Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya amesisitiza lazima tuwahakikishie tunawapa vijana wetu silaha zote za wao kwenda kwenye mapambano duniani, kwa kuwafunza matumizi sahihi ya Tehama ili kushindana katika soko la dunia pia kupambana na changamoto ya kasi ya dunia ya sasa na ya baadae.

Naye Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Ngudu Donatus Richard amesema wao ni wadau wakubwa wa maendeleo na wamekabidhi Mabati 222, Mbao 420 pamoja na Kilo 410 za misumari ili kufanikisha kuwezekwa kwa mabati katika shule hizo lengo kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Kwa namna yake Mkuu wa Shule ya Buza Ndugu Michael Kabuta ameongea kwa niaba ya shule zote huku akitoa shukrani zake za dhati kwa NMB kwa kuwakabidhi vifaa hivyo na kutoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kuunga mkono serikali katika kusaidia taasisi mbali mbali zenye uhitaji wa namna hiyo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke