• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

"TUNAMSHUKURU SANA MHE. RAIS KWA KUTUPUNGUZIA MZIGO'' MSTAHIKI MEYA TEMEKE

Posted on: November 19th, 2021


Novemba 19,2021 Meya wa halmashauri ya manispaa ya Temeke mheshimiwa Abdallah Mtinika ameendesha baraza la madiwani kwa robo ya kwanza(Julai-Septemba) baraza lililohudhuriwa na maafisa kutoka taasisi za Umma ikiwemo TANESCO na DAWASA, huku mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo na mkurugenzi wa manispaa ndugu Elihuruma Mabelya wakihudhuria kwa mara ya kwanza.

Katika kikao hicho mstahiki meya Mtinika amepokea taarifa kutoka Kata,kufafanua ajenda muhimu za Manispaa na kutoa shukrani za dhati kwa rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za UVIKO -19 kiasi cha Shilingi Bilioni 3.4 kwa Manispaa ya Temeke kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 157 vya madarasa.


"Tunamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupunguzia mzigo tuliokua nao na kuongeza lengo kwa sababu tulikua na mpango wa kujenga vyumba vya  madarasa 145, fedha hizi zimetufikisha madarasa 157.


Na kwa suala la kuwapanga wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) halmashauri yetu imefanya vizuri, ajenda inayofuata ni kusafisha mji wetu.


Katika baraza hili pia tumeanza kuonesha matunda ya muungano wa kitaasisi hasa kwa baadhi ya taasisi zinazotoa huduma kwa Wananchi kwa maana tukikutana ndipo tunaijenga Temeke yetu kwa kujua vipaumbele vya Wananchi na hii ndiyo Tanzania ya mama Samia Suluhu Hassan." Alisema Mhe. Mtinika.


Aidha Mhe. Mtinika ametoa wito kwa taasisi zote zilizopo Temeke kutenga muda wa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani ili kuungana kusaida serikali na kuwatumikia Wananchi kwa namna inayofaa.


Kwa upande wake mkurugenzi Mabelya  ametoa shukrani zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kueleza hali ya ujenzi wa madarasa Temeke ambapo amesema.


"Hali ya ujenzi wa vyumba vya madarasa iko vizuri na tunatarajia kufikia Disemba 08 tutakua tumepaua vyumba vyote".


Naye mkuu wa wilaya Mhe. Jokate Mwegelo amemshukuru Mhe. Mtinika na madiwani kwa ujumla kwa kumualika kwa mara ya kwanza kuhudhuria baraza hilo. Alisema


"Nipende kukushukuru Meya Mtinika na baraza lako kwa jinsi mnavyoendesha Manispaa yetu,nashukuru kwa kunialika na kunitambulisha,naendelea kusisitiza tufanye kazi kwa umoja,ushirikiano na mshikamano,tuendelee kusimamia ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa faida ya Wananchi"


Baraza la madiwani limeanzisha utaratibu wa kualika taasisi zinazohudumia Wananchi moja kwa moja ili kuleta msukumo kwa taasisi hizo kupata maoni kutoka kwa madiwani ambao ni wawakilishi wa Wananchi, lengo ni kuhakikisha matakwa  yanatimizwa.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA BAADA YA USAILI KWA AJILI YA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE March 05, 2025
  • TANGAZO MUHIMU July 14, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 19, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 30, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SHEREHE YA WALIMU YAFANA TEMEKE

    April 25, 2025
  • MEYA AZUNGUMZA MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • HAFLA YA UTOAJI MIKOPO, RC AKABIDHI HUNDI

    April 24, 2025
  • RC ANENA KATIKA HALFA YA UTOAJI MIKOPO YA 10%

    April 24, 2025
  • Angalia zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA RASIMU YA BAJETI 2025/2026
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke