• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Temeke Municipal Council
Temeke Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii, na Vijana
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi na Mipango miji
      • Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Uhusiano na Teknolojia ya Habari
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki na wanyama pori
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Utoaji wa Leseni za biashara
    • Utoaji wa Leseni za vileo
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
    • Utoaji wa hati na leseni za Makazi
    • Utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi (10%)
    • Upimaji wa ardhi
    • Usajili wa vikundi vya kijamii
    • Uandikishaji wa bima ya afya ya jamii (iCHF)
    • Utoaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
    • Kulipia ushuru na tozo za Halmashauri
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za wahesimiwa Madiwani
      • Kamati ya fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango miji na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya maadili
    • Siku ya kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Vipeperushi
    • Mpango Mkakati wa Manispaa
    • Sheria ndogo
    • Miongozo mbalimbali
    • Ripoti
  • Chanzo cha habari
    • Gazeti Mtandao
      • Toleo Mei 2,2021
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
  • Nyaraka
    • Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma
  • Mifumo

WAATHIRIKA 1300 WA MADAWA YA KULEVYA WAPATIWA HUDUMA YA METHADONE KWA SIKU TEMEKE

Posted on: February 3rd, 2023

Na: Nassoro Rashid   TMC Habari

Leo Februari 3, 2023 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Temeke ambaye pia ni Naibu Meya wa Halmashauri Mhe. Anorld Peter ameongoza kamati hiyo katika ziara ya kutembelea vituo vya utoaji wa huduma ya afya ya akili na methadone  vilivyopo katika Manispaa hii.

Akizungumza wakati akiwa katika kituo cha Methodone kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa  Temeke, Mhe. Anorld ameupongeza uongozi wa kituo hicho kwa utoaji wa huduma bora na za kisasa kwa waathirika hao ambao mpaka sasa kituo hicho kimefanikiwa kuwasajili waathirika 2904 kwa ajili ya huduma hizo.

"Kipekee niwapongeze sana Mganga Mfawidhi na jopo lako lote, watu 1300 wanapewa huduma kwa siku si idadi ndogo, na Serikali imejipambanua kutoa huduma bora kwa Wananchi wake, mmetueleza hapa kwamba  mmetoka kwenye mfumo wa kizamani na sasa mpo mfumo wa kisasa wa kutoa huduma, lakini kupokea wagonjwa  2904 sio mchezo, sisi kama kamati lazima tuwape nguvu ya kuwahudumia Wananchi hao." Alisema Mhe. Anorld.

Akijibu hoja ya Mganga Mfawidhi kuhusu changamoto ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utoaji wa huduma za mikojo, usafishaji wa figo pamoja na damu,Mhe. Anorld amesema,

"Kuna changamoto mmezisema hatuwezi kuzijibia hapa, ila tunazibeba ili tuzipeleke katika vikao tuweze kujadili kwa pamoja, wapo Madiwani hapa, tutakwenda kupata ushauri wa Menejimenti na kuweza kuamua, huu mradi wa kusafisha figo, damu na huduma za mkojo ni mzuri sana lakini mmekosa eneo, hivyo tunawaahidi kulifanyia kazi hili ili tupate mwafaka." Alisema Mhe. Anorld

Aidha Mhe. Anorld amesema  kwamba suala  la uongozi kuwatafutia fursa na shughuli mbalimbali za kufanya wagonjwa ambao wanaonesha mwelekeo mzuri wa kupona ili kuwaondoa katika vishawishi vya kurudia matumizi ya madawa ya kulevya ni maono mazuri,yapaswa kuigwa na kupewa nguvu.


Matangazo

  • TANGAZO: KUFUNGA VITUO VYA DAYCARE January 29, 2023
  • TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA January 06, 2023
  • TANGAZO: KUWASILISHA HESABU (TURNOVER) February 13, 2023
  • TANGAZO: KUWASILISHA HESABU (TURNOVER) February 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • KILIO CHA KIVUKO KATA YA MIANZINI CHAFIKA MWISH0

    March 25, 2023
  • "TUTAPAMBANA NA KIPINDUPINDU KWA USAFI" MHE. AMOS MAKALLA

    March 25, 2023
  • MTAKUWWA TEMEKE YADHAMIRIA KUDHIBITI VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO

    March 24, 2023
  • WANAHABARI WANA JUKUMU LA KUELIMISHA JAMII KUHUSU UGONJWA WA KIFUA KIKUU-MHE. UZAHILU

    March 24, 2023
  • Angalia zote

Video

RC MAKALLA AONGOZA ZOEZI LA USAFI MBAGALA
Picha jongefu za ziada

Kurasa za Karibu

  • YouTube
  • Vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Salary Slip Portal
  • Email za watumishi wa serikali TemekeMC (GMS)
  • National WASH Data Platform
  • Instagram
  • Facebook

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Taifa
  • TANEPS
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Utumishi
  • Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Manispaa ya Temeke inapatikana mkabala na uwanja wa Taifa katika makutano ya barabara ya Mandela na Taifa.

    Anuani ya Posta: P.O.Box 46343 Dar-es-Salaam

    Simu ya Mezani: +255 22-2928132

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: temeke@temekemc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Mtandao

Hatimiliki©2018. Halmashauri ya Manipaa ya Temeke